Wachezaji wa Mbuyuni Market FC wakimpongeza mfungaji wao Joram Maingu (9) aliyetupia bao pekee la ushindi katika dakika ya 25 dhidi ya Mweta FC ya Mwanza |
Miamba ya Soka mkoa wa Kilimanjaro Mbuyuni Market imepata ushindi wake wa kwanza katika kinyang’anyiro cha kupanda Ligi Daraja la Pili msimu ujao katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) dhidi ya Mweta FC kutoka Mwanza kwenye mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Ushirika Mjini Moshi.
Mchezo huo wa kundi B katika kituo cha Kilimanjaro ulishuhudiwa nyota wa Mbuyuni Market Joram Maingu akiipatia bao pekee timu yake katika dakika ya 25 akiwahadaa walinzi wa kati wa Mweta FC na kufumua mkwaju uliojaa wavuni.
Katika mchezo huo ulishuhudiwa dakika 20 kabla ya kuanza mvua kubwa ilinyesha ikitishia kutochezwa kwa mchezo huo, hata hivyo uliochezwa na timu zote mbili zikionyesha ustadi mkubwa katika dimba hilo.
Mbuyuni Market ilipoteza katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi dhid ya Mufeza United ya Tanga.
STORY & PHOTO BY: Jabir Johnson
EMAIL: jabirjohnson2020@gmail.com
DATE: Machi 16, 2020
Mvua ilianza kunyesha saa 9:36 alasiri na kuendelea hadi saa 11:26 jioni |
Hekaheka langoni mwa Mweta FC |
Hekaheka langoni mwa Mbuyuni Market |
Dakika nne ziliongezwa kumaliza mchezo huo baina ya Mweta FC na Mbuyuni Market. |
0 Comments:
Post a Comment