Tuesday, July 7, 2020

Historia ya SabaSaba Day ya Tanzania

Maonyesho ya SabaSaba yamekuwa yakifanyika kila mwaka nchini Tanzania Julai 7 yakiwa na kaulimbiu mbalimbali kila mwaka. 

Maonyesho hayo ya biashara yanayojulikana kama SabaSaba yalianza mwaka 1962 yakiwa ni maonesho ya Kilimo yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Wizara ya Biashara na Ushirika. Maonyesho hayo yalikuwa na lengo la kukuza kilimo na ushirika.

Mwaka 1978 serikali iliunda Bodi ya Biashara ya nje kupitia sheria yake namba 5 ya mwaka huo, Bodi hiyo ilipewa mamlaka kushughulikia usafirishaji wa bidhaa za kitanzania nje ya nchi. Bodi ya Biashara ya nje ilipewa pia dhamana ya kukuza ushirikiano wa biashara ya kimataifa kupitia maonesho ya kibiashara, kufanya utafiti kuhusiana na biashara.

Miaka ya hivi karibuni maonesho hayo yamekuwa yakishirikisha nchi takribani 20 kutoka kusini mwa Afrika (SADC) vilevile yamejulikana kama maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam na viwanja vinajulikana kama viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere. 

0 Comments:

Post a Comment