Wednesday, July 1, 2020

Ufahamu mwezi Julai

Julai ni mwezi wa saba katika mtiririko wa miezi kwenye kalenda ya Gregori na ile ya Julian. 

Julai ni mwezi uliopo kati ya Juni na Agosti, pia ni mwezi wa nne kati ya saba yenye siku 31. Julai ni mwezi ulipatiwa jina na baraza la Seneti la Rumi kwa heshima ya Jenerali wa Kirumi Julius Caesar.

Sababu kuu ilikuwa ni kwamba mwezi huu ulikuwa ndio mwezi aliozaliwa mtawala huyo maarufu katika historia ya Rumi. Kabla ya hapo katika kalenda ya zamani ya Kirumi iliyokuwa na miezi 10, Julai ulikuwa ukifahamika kwa jina la Quintilis. Pia katika kalenda hiyo ulikuwa ni mwezi wa tano kati ya miezi 10.

Katika Rumi ya zamani kulikuwa na sherehe mbalimbali ambazo zilikuwa zikisherehekewa ikiwamo ya Poplifugia ambayo ilikuwa ikifanyika kila Julai 5 na Ludi Apollinares kwa ajili ya mungu Apollo ilikuwa ikifanyika Julai 13 kila mwaka.  

Licha ya kwamba tarehe hizo katika kalenda ya kisasa ya Gregori hazikuingizwa.


0 Comments:

Post a Comment