Michirizi katika sehemu za mwili imekuwa ikitamkwa na wengi kama ‘stretch marks’ ambapo hutokea sehemu mbalimbali mwilini kama mikononi, miguuni, mapajani au tumboni.
Michirizi na mikunjokunjo kwenye ngozi ya mapaja, tumbo na kwenye mikono ni tatizo linalowatesa zaidi wanawake.
Wengi wanahangaika ili kuondokana na tatizo hili bila mafanikio. Pamoja na kutumia vipodozi na cream mbalimbali bado tatizo halijaisha.
Tatizo linawafanya kina dada kuona aibu, kushindwa kujiachia na kutovaa nguo wanazozitaka kwa kuogopa mikunjo kuonekana.
Baadhi ya vitu vinavyosababisha mikunjokunjo kwenye ngozi ni
pamoja na kuvurugika kwa homoni, pamoja na kutokufanya mazoezi. Tatizo hili
huwatokea zaidi wanawake kuliko wanaume kutokana na unene kupita kiasi ambapo
sehemu ya ndani yenye mafuta (fat globules) inakua na msuguano na tishu za
ngozi na hivyo mikunjokunjo na michirizi kwenye ngozi hutokea.
CHANZO CHA MIKUNJO NA MICHIRIZI
Sababu zinazochangia upate mikunjokunjo na michirizi kwenye ngozi ni pamoja na Lishe mbovu, Mwili kubakiza maji tumboni (fluid retention ambapo wakati mwingie hupelekea tumbo kujaa gesi),
Damu kutozunguka vizuri, Udhaivu wa tishu zenye Collagen (collagen ni kiungo kilichosheni protini ambacho kinatengeneza shape na tishu za ngozi. Hivyo kufanya ngozi ya mtu kuonekana bado changa) na kufanya kujikunja kiurahisi, Mabadiliko ya homoni, Mwili kukosa mazoezi na kutoshugulika.
Pia msongo wa mawazo kupita kiasi ambao hupunguza uzalishaji wa collagen, na Historia ya magonjwa mfano magonjwa ya autoimmune, kisukari, watu wanaovuta sigara na wenye alegi/mzio husababisha mikunjo na michirizi hiyo.
Kwa kawaida, michirizi haimletei mtu maumivu yoyote, bali jambo kubwa huwa ni kuubadili muonekano wa ngozi ya mtu.
Ikifikia hatua
hii kwa namna moja au nyingine humnyima mtu uhuru au humfanya mtu asiwe na
amani anapokuwa mbele ya watu kwa kutegemea michirizi hiyo imetokea sehemu gani
ya mwili.
0 Comments:
Post a Comment