Waislamu wa Sunnia na Shia wanakubaliana katika maeneo
mengi hususani misingi ya imani ya dini ya Kiislamu kutoka kwa mwanzilishi wao
Mtume Muhammad S.A.W
Hata hivyo kutofautiana kwao tunarudi nyuma yapata
karne kama 13 zilizopita. Tofauti za kimsingi zinaanza katika matendo yao kwani
Wasunni wamelalia kwenye Sunnah yakiwa ni rekodi ya mafundisho na misimamo ya Mtume
Muhammad huku Washia wakijikita sana kwa Maayatolla (ayatollahs) kama ishara ya uwepo wa Mungu duniani.
Duniani hii leo asilimia 85 ya Waislamu ni wale
wanaofuata misimamo ya Kisunni na asilimia 15 tu ni Washia. Takwimu mbalimbali zinaweka bayana kwamba Washia walio wengi wapo katika nchi za Iran, Iraq,
Bahrain na Azerbaijan. Pia Yemen, Bahrain, Syria na Lebanon.
Wasunni walio wengi wamesambaa zaidi ya nchi 40 kutoka Morocco hadi Indonesia. Miongoni mwa nchi zilizokaliwa na Wasunni ni Saudi Arabia, Misri, Yemen, Pakistan, Indonesia, Turkey, Algeria, Morocco, na Tunisia
Licha ya tofauti zao kwa miaka mingi wamekuwa wakiishi kwa amani lakini mapema
mwanzoni mwa karne ya 20 kulianza vuguvugu na visa vyenye ukali katika baadhi
ya maeneo huko Mashariki ya Kati kwa ajili ya kuwania nafasi katika dini na
siasa.
Mizizi ya mgawanyiko wa Sunni-Shia inaweza kupatikana
wakati wote kurudi karne ya saba, mara tu baada ya kifo cha Mtume Muhammad
mnamo mwaka 632. Wafuasi wengi wa Muhammad walidhani baadhi yao wanapaswa
kuchagua mrithi, kikundi kidogo kiliamini mtu pekee kutoka kwa familia ya
Muhammad yaani binamu yake na mkwewe. Turufu hiyo ilimwangukia Ali kuwa mrithi
wa mikoba ya Mtume. Kikundi hiki kilijulikana kama wafuasi wa Ali; kwa Kiarabu
Shiat Ali, au Shia.
Mwandishi wa Kitabu “After the Prophet: The Epic Story
of the Sunni-Shia Split in Islam” Lesley Hazleton aliandika, “Kiini cha shida hii
ni kwamba Muhammad alikufa bila mrithi wa kiume, na hakuwahi kusema wazi ni
nani atataka kuwa mrithi wake.”
Hazleton alisema kuwa hatua hiyo ilikuwa muhimu
kwasababu wakati anafariki dunia Mtume Muhammad alikuwa amefanikiwa pakubwa
kuyaweka pamoja makabila yote ya Arabia na kufanya kile kinachoitwa Ummah yaani
mamlaka ya watu au taifa la Kiislamu.
Walio wengi walimchagua rafiki wa karibu Abu Bakr kuwa
Khalifa wa kwanza katika jamii ya Waislamu. Ali alikuja kuwa Khalifa wanne au Imam
ikiwa ni baada ya wawili waliomtangulia kuuawa.
Ali aliuawa mwaka 661, hivyo makundi mawili
yakajitokeza ambao ni Wasunni na Washia. Karne moja baadaye baada ya kifo cha
Mtume Muhammad makundi hayo yalijitanua hadi Kutoka Central Asia hadi Hispania.
Mnamo mwaka 681 mtoto wa Ali aliyefahamika kwa jina la
Hussein aliongoza kundi la watu 72 kutoka Makka hadi Karbala (ipo Iraq) kwa
ajili ya kuuondoa utawala uliojaa rushwa wa Yazid kutoka ukoo wa Ummayad.
Majeshi ya Kisunni yalikuwa yakiwasubiri ambako kulipiganwa vita ya siku 10.
Mwishoni mwa vita hiyo Hussein aliuawa na mafuasi wake kuondolewa kisha kicha
chake kilikatwa na kupelekwa Damascus kwa Khalifa wa Kisunni.
Walichokifanya Wasunni ilikuwa ni kulipoteza kabisa
kundi na wafuasi wa Hussein lakini haikuwa hivyo kwani katika utamaduni wa
Kishia wanamtazama Hussein kama kioo chake na wanampa heshima yake kupitia
kalenda yao Kishia kama siku ya Ashoura kutokana na juhudi zake alizozifanya
hapo Karbala.
Waislamu wa Shia wanaamini kuwa Imam hana dhambi kwa asili
na kwamba mamlaka yake haina maana kwa sababu inatoka moja kwa moja kutoka kwa
Mungu. Kwa hivyo, Waislamu wa Shia mara nyingi huabudu Maimamu kama watakatifu.
Wao hufanya Hija katika makaburini na wakiwa na matumaini ya maombezi ya Mungu.
Kwa upande wao Waislam wa Sunni wanapinga kwamba
hakuna msingi katika Uislam kwa kikundi cha baraka cha viongozi wa kiroho, na kwa
kweli hakuna msingi wa kuabudu au kuombewa kwa watakatifu. Wanashikilia kwamba
uongozi wa jamii sio haki ya kuzaliwa, lakini ni uaminifu unaopatikana na unaoweza
kupewa au kuchukuliwa na watu.
Waislam wa Kisunni na Shia wanafuata Quran na vile
vile hadithi za Mtume (SAW) na Sunna (mila). Hizi ni mazoea ya kimsingi katika
Imani ya Kiisilamu. Pia wanafuata nguzo tano za Uislam: shahada, salat, zakat,
sawm, na hajj.
0 Comments:
Post a Comment