Sunday, June 21, 2020

Mfahamu Sukarno, baba wa taifa la Indonesia


Juni 21, 1970 alifariki dunia mwasisi wa taifa la Indonesia Sukarno. Alifariki dunia akiwa nyumbani kwake mjini Jakarta. Alifariki dunia kwa maradhi ya figo akiwa na umri wa miaka 69. Alizikwa huko Blitari, Mashariki ya Java kwa heshima.

Sifa yake kubwa alikuwa na uwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu  pia alikuwa na kipaji cha kuzijua lugha ikiwamo Kijava, Kibali, Kisunda, Kiholanzi, Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kibahasa cha Indonesia, Kijerumani na Kijapan. Sukarno badala ya kuunga mkono mfumo wa asili wa bunge na aliunda mfumo mwingine wa kidemokrasi lakini ukiwa mikononi mwake.

Mwaka 1965 Sukarno aliondolewa kwa nguvu za kijeshi na ukawa mwisho wake wa kukalia kiti cha kuliongoza taifa hilo. Alizaliwa Juni 6, 1901 katika Java wakati kisiwa hicho kilipokuwa mali ya Dutch East Indies, Sukarno aliibuka na kuwa mwenye nguvu mwaka 1949.

Sukarno alikuwa kiongozi mashuhuri wa harakati za ukombozi wa Indonesia wakati wa wakikaliwa kwa mabavu na Waholanzi. Katika mapambano hayo aliwekwa kizuizini kwa zaidi ya miaka 10 hadi alipotolewa na vikosi vya Japan vilivyovamia katika Vita vya Pili vya Dunia. Sukarno na raia wenzake walishirikiana kupata msaada kutoka Japan ambayo ilisaidia kueneza maoni ya uzalendo wa taifa hilo.

Sukarno na Mohammad Hatta walitangaza uhuru wa Indonesia mnamo Agosti 17, 1945, na Sukarno aliteuliwa kama rais wa kwanza wa taifa hilo. Aliwaongoza Waindonesia katika kupinga ukoloni wa Uholanzi kwa njia za kidiplomasia na kijeshi hadi kutambuliwa kwa Uholanzi juu ya uhuru wa Indonesia mnamo 1949.

Mwandishi Pramoedya Ananta Toer aliwahi kuandika, "Sukarno alikuwa kiongozi wa pekee wa Asia ya enzi ya kisasa aliyeweza kuunganisha watu wa kutofautiana kama hii. asili, kitamaduni na kidini bila kumwaga tone la damu. "

Enzi za uhai wake alifanikiwa kuzaa watoto watano ambao ni Sukarno, Sukmawati, Fatmawati, Guruh, Megawati, Guntur, Rachmawati. Sukarno alioa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1920 na kuishi na Siti Oetari. Mwaka 1923 waliachana kisha Sukarno akamwoa Inggit Garnasih ambaye walitalikiana mnamo mwaka 1943. Hakuishia hapo alimwoa Fatmawati ambaye waliachana bila talaka (walitengana).

Mnamo mwaka 1954 alimwoa Hartini. Ilipofika mwaka 1959 alimtambulisha mwanadada wa Kijapan mwenye umri wa miaka 19 Naoko Nemoto ambaye alimwoa mnamo mwaka 1962. Alipomwoa alimbadilisha jina na akawa anaitwa Ratna Dewi Sukarno. 

Sukarno aliwaoa wanawake wengine wanne kutoka mwaka 1963 hadi 1969. Haryati (1963–1966); Kartini Manoppo (1959–1968); Yurike Sanger (1964–1968); Heldy Djafar (1966–1969). Sukarno kwa asili ni wa kizazi cha Wajava na Wabali.

0 Comments:

Post a Comment