Monday, June 1, 2020

Ufahamu mwezi Juni



Juni ni mwezi wa sita katika mwaka hususani katika Kalenda ya Gregori. Huu ni mwezi uliopo kati ya Mei na Julai. Juni una siku 30. Juni ulipewa jina hilo kutokana na Mungu mke wa Warumi aliyeitwa Juno na Mungu mume aliitwa Jupita. 

Hivyo basi unaweza kumwelezea Juno kuwa alikuwa mke wa Jupita. Kwa Kilatini mwezi huu hufahamika kama Junius. Juno alikuwa Mungu wa masuala yanayohusu Ndoa. Juno alijikita katika kutungwa kwa mtoto na kuzaliwa kwa mtoto. Hakuna mwezi ambao katika mwaka huwa unaanza siku moja na wiki lake kama ulivyo mwezi Juni. Pia mwezi huu humalizikia siku moja na wiki lake kama ulivyo mwezi Machi katika miaka yote. 

Kwa mfano mwezi Juni mwaka 2020 unamalizikia siku ya Jumanne ambayo ni Jumanne ya Juni 30, sasa mwezi Machi nao huwa unamalizikia siku kama hiyo hiyo kama ulivyo Juni. Kwa mantiki hiyo Juni 30, 2020 ni siku ya Jumanne ambayo ni sawa na Machi 31, 2020 ambayo ni Jumanne. 

Pia ukitazama hilo kwa makini utagundua kuwa ni kwa miaka yote siku ya mwisho ya mwezi Juni inafanana na ile ya mwezi Machi kila mwaka. Mfano Juni 30, 2021 ni Jumatano ambayo ni sawa na Machi 31, 2021 ambayo ni Jumatano. 

Juni unafanana pia na mwezi Februari kwa mwaka unaofuata namna unavyoanza. Kwa mfano mwaka 2020 tarehe 1 ya mwezi Juni ni siku ya Jumatatu hivyo basi siku ya kwanza ya mwezi Februari mwaka 2021 ni Jumatatu kama ilivyo Juni 2020. 

0 Comments:

Post a Comment