Juni 12, 1964 Nelson
Mandela, mwanasiasa maarufu nchini Afrika Kusini na duniani kwa ujumla ambaye
alikuwa mtu muhimu katika kuutokomeza ubaguzi wa rangi nchini humo alihukumiwa kifungo
cha maisha kutokana na harakati hizo. Kwa ufupi ni kwamba alianza kutumikia
kifungo cha miaka 27 jela.
Mandela alikuwa mtoto wa Chifu wa
kabila la Tembu, Chifu Henry Mandela. Mandela alizaliwa katika kijiji cha Mveso
kwenye mji mdogo wa Transkei, Julai 18, 1918.
Mandela alikamatwa, akatiwa hatiani
na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani kuanzia mwaka 1964 hadi 1990, ambapo
maisha yake kama kiongozi wa harakati za kupambana na ubaguzi wa rangi
yakajulikana dunia nzima. Kama mfungwa wa dhamiri, Mandela mara kwa mara
alikataa kuachiwa kwa masharti.
Mwaka 1990, akiwa amekaa jela kwa
miaka 27 na akiwa na umri wa miaka 71, iliachiwa huru bila masharti yoyote
baada ya utawala wa kibaguzi kushinikizwa na jumuiya ya kimataifa.
Mwaka 1993, Nelson Mandela
alishinda Tuzo ya Nobel kwa harakati zake za kisiasa. Mwaka 1994 akiwa katika
umri huo, Mandela aligombea kiti cha urais na kushinda akiwa rais wa kwanza
mweusi.
Mwaka 1944, alijiunga na chama cha
siasa cha African National Congress (ANC), kilichoundwa kwa lengo la
kukabiliana na sera za ubaguzi wa rangi za serikali ya wachache ya nchini
Afrika Kusini iliyoongozwa na watu weupe.
Na baadaye, mfumo huu ukabadilika
na kuwa mapambano ya muda mrefu dhidi ya ubaguzi yaliyoongozwa na Mandela. Nelson
Mandela aliunda tawi la kijeshi ndani ya ANC lililojulikana kama "Umkhonto
we Sizwe" au "Mkuki wa taifa" ili kukabiliana na serikali
iliyoko mamlakani na sera zao za ubaguzi wa rangi.
Alishitakiwa kwa hujuma na kupanga
njama za kuipindua serikali mnamo mwaka 1964, na ndipo alipofungwa kifungo cha
maisha katika gereza lililopo kwenye kisiwa cha Robben.
Mandela alikivutia kizazi cha
Afrika Kusini kwa kuwa ingawa alikuwa kifungoni kwa muda mrefu, utu wake na
mtizamo wake juu ya ulimwengu ulipenya hadi nje ya kuta za gereza.
Miongo kadhaa aliyotumikia kifungo
haikumvunja nguvu, bali ilimjengea mchango wake wa kihistoria katika mapambano
ya kusaka uhuru wa taifa hilo.
0 Comments:
Post a Comment