Juni 24, 1908 alifariki dunia mwanasiasa na Rais wa 22 na 24 wa
Marekani Grover Cleveland. Alifariki dunia huko Princeton, New Jersey, akiwa na
umri wa miaka 71.
Cleveland ni miongoni mwa Marais waliozama ikulu ya White
House wakiwa hawajaoa yaani (mabachela au makapera) mwingine ni James Buchanan.
Akiwa na umri wa miaka 47aliingia ikulu na dada yake Rose
Cleveland aliungana naye ili amsaidie baadhi ya kazi katika miaka miwili ya
kwanza katika utawala wake. Hata hivyo Cleveland hakukaa sana katika ukapera
kwani mnamo mwaka 1885 binti wa rafiki yake Oscar Folsom alimtembelea Washington.
Mwanadada huyo alifahamika kwa jina la Frances Folsom ambaye alikuwa mwanafunzi
wa Chuo cha Wells.
Wakati alipokuwa akirudi chuoni kuendelea na masomo Rais Cleveland alipata ruhusa kutoka kwa mama yake kuwa anaweza kuingia naye mahusiano na haikupita muda wakaoana.
Juni 2, 1886 Cleveland akiwa na umri wa miaka 49
alimwoa mwanadada Frances ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 21 Chumba
kimoja kati ya vitatu katika Ghorofa ya Juu ya White House kinachofahamika kama
‘Blue Room’.
Cleveland aliweka rekodi ya kuwa Rais wa pili wa Marekani kufunga
harusi katika Ikulu ya White House. Mwanadada
Frances akiwa na umri wa miaka 21 aliweka rekodi ya kuwa First Lady mwenye umri
mdogo kuwahi kushika wadhifa huo katika historia ya taifa hilo na aliwavutia
awengi sana.
Cleveland alizaa watoto watano Ruth (1891–1904), Esther
(1893–1980), Marion (1895–1977), Richard (1897–1974), na Francis (1903–1995). Mwanafalsafa
wa Uingereza Phillipa Foot ni mjukuu wa Cleveland. Cleveland alikuwa rais pekee
katika historia ya Marekani kuliongoza taifa hilo katika vipindi viwili
tofauti.
0 Comments:
Post a Comment