Juni 16, 1958 mwanasiasa wa
Kikomunisti wa Hungaria Imre Nagy alinyongwa kwa makosa ya uhaini baada ya
Urusi kunyakua tena ardhi ya Hungaria.
Nagy alihudumu katika nafasi ya
Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri
wa Jamhuri ya Watu wa Hungaria kutoka mwaka 1953 hadi 1955. Nagy
alinyongwa akiwa na umri wa miaka 62 huko Budapest, Hungaria.
Mwanasiasa huyo ameendelea
kuwavutia wengi ambapo mwaka 2003 na 2004 mkurugenzi wa filamu na mwongozaji Marta Meszaros
alitengeneza filamu kumhusu Nagy ikijikita katika maisha yake baada ya
mapinduzi. Filamu hiyo ilipewa jina la ‘ A temetetlen halott’ ikiwa na maana
Mwili ambao Haujazikwa.
Pia Nagy ametajwa katika filamu
nyingine ya Children of Glory ilitoka mwaka 2006 iliongozwa na Krisztina Goda.
Wakati wa utawala wa Stalin nchini Hungaria ilikuwa hairuhusiwi kufanya
kumbukizi au kwenda kwenye makaburi kwa ajili ya marehemu wao, hata hivyo mnara
wa kaburi tupu ulijengwa jijini Paris katika makaburi ya Père Lachaise Juni 16,
1988.
Mnamo mwaka 1989 mabaki ya Nagy
yalizikwa upya katika kumbukizi ya 31 katika eneo hilo alilozikwa kwenye
mazishi yalioongozwa na upande wa Demokratiki nchini huo uliokuwa ukipinga
utawala wa Stalin.
Zaidi ya watu 200,000 walihudhuria
maziko hayo. Mazishi ya Nagy ilikuwa ni nukta muhimu katika miaka ya miwshoni
ya utawala wa Kikomunisti nchini Hungaria. Katika hali ya kustaajabisha mnamo Desemba 28,
2018 sanamu maarufu ya Nagy iliondolewa katikati ya jiji la Budapest na
kupelekea nje kidogo.
Vyama vya upinzani vyenye misimamo
ya Kiliberali na Kisoshalisti viliendelea kumlaumu waziri mkuu mwenye mrengo wa
kulia Victor Mihaly Orban kwa kuiondosha sanamu hiyo.
Katika siasa, Nagy alianza tangu
mwaka 1917, lakini baada ya vita vikuu vya pili vya dunia alirudi nchini
Hungaria. Aliteuliwa kuwa waziri wa Kilimo katika serikali ya Bela Mikols de
Dalnok kwa tiketi ya Chama cha Kikomunisti.
0 Comments:
Post a Comment