Thursday, June 18, 2020

Namna ya Kupambana na maradhi ya Kupoteza Kumbukumbu (Dementia)


Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu kwa kitaalamu unafahamika kama dementia (demenshia).  Watu wenye umri zaidi ya miaka 65 wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huu.

Dalili za ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu zinaweza kuwa: 

1. Kupoteza kumbukumbu-Kusahau mambo, njia ya kurudi nyumbani, kusahau watu,  kutokumbuka mazungumzo na kurudiarudia maneno.

2. Mabadiliko katika haiba-Kukosa raha, woga au hasira juu ya mambo yanayo watokea. Matatizo katika mawasiliano-Kushindwa kupata maneno sahihi ya kuzungumza au majina sahihi ya vitu.

Katika hatua za mwisho za ugonjwa huu, mgonjwa hushindwa kufanya shughuli za kila siku na anazidi kuwa tegemezi kwa watu wengine.

VISABABISHI VYA DEMENTIA

Hii inaweza kusababishwa na kiharusi kutokana na shinikizo la damu. Ziko sababu nyingine nyingi kama vile kusinyaa kwa ubongo, unywaji wa pombe nyingi, Ukimwi nk.

Baadhi ya visababishi hivi vinatibika au kuzuilika. Hivyo ni muhimu kwenda hospitalini kwa ushauri zaidi.

MATOKEO YA DEMENTIA 
Unasababisha mtu kupoteza uwezo wa kuelewa, unaathiri kumbukumbu, mawazo, uwezo wa kujifunza, lugha na unatokana na baadhi ya magonjwa au majeraha ambayo yanaathiri ubongo. 

Takwimu za mwaka 2019 za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zilionyesha kuwa kuna wagonjwa takriban milioni 50 wa kupoteza kumbukumbu kote duniani    idadi ambayo inatarajiwa kuongezeka mara tatu ifikapo mwaka 2050.

NAMNA YA KUJIKINGA 
Shirika la afya ulimwenguni WHO lilitoa mwongozo mpya wa kusaidia watu kupunguza hatari za ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu, ambao pamoja na mambo mengine unataja masuala kama vile kufanya mazoezi mara kwa mara, kutovuta sigara, kuepuka matumizi hatarishi ya vileo na lishe bora. 

0 Comments:

Post a Comment