Juni 14, 1830 Wafaransa walianza rasmi kulitawala taifa la Algeria kwa mabavu. Ufaransa ilianza kwa kupeleka wanajeshi 34,000 ambao walianza kuvamia eneo la kilometa 27 kusini mwa eneo la Sidi Ferruch.
Uvamizi wa Ufaransa katika ardhi ya Algeria kwa mara ya kwanza ulianzishwa katika siku za mwisho za maisha za Mtawala wa Ufaransa Charles X. Alifanya hivyo ikiwa ni mpango wake wa kujiongezea umaarufu kwa Wafaransa hususani wa Jiji la Paris ambako maveterani wengi wa Vita vya Napoleoni walikuwa wakiishi.
Makusudi yake makuu yalikuwa ni kuongeza chembechembe za uzalendo wa kulipenda taifa la Ufaransa pia kuvuruga usikivu na ufuatiliaji wa sera za ndani.
Awali kabisa kabla ya mpango huo wa kuvamia Algeria, kulikuwa na mahusiano mazuri ya kibiashara baina ya Wafaransa na wakazi wa Algeria waliokuwa wakifanya biashara ya ngano.
Mwishoni mwa miaka ya 1790 wafanyabiashara wawili wa Algeria waliuza ngano yao katika Jeshi la Kifaransa. Waalgeria hao ambao walikuwa wenyeji wa Algiers huko Messrs wanatajwa kwa majina kuwa ni Bacri na Boushnak walikuwa na deni ambalo walidai kuwa hawana uwezo wa kulipa mpaka Ufaransa itakapowalipa madeni inayowadai.
Msuluhishi wa Ufaransa Pierre Deval aliitisha meza ya mapatano baina ya pande zote mbili lakini hakufanikiwa kwa alikuwa akidhaniwa kuwa alikuwa upande wa Wafanyabiashara wa Kialgeria.
Binamu yake aliyefahamika kwa jina la Alexandre aliyekuwa akisimamia eneo la Bone alikasirika kwa kushindwa kufikia makubaliano. Ukaitishwa mkutano ambao uliwakutanisha na Deval ambaye alikataa kutoa majibu Aprili 29, 1827 hatua iliyopelekea kupigwa na mkongojo wake (fly-whisk).
Charles X alitumia nafasi hiyo na kuomba radhi kwa kilichotokea na baada ya hapo alitia saini mpango wa kuihusuru bandari ya Algiers. Wafaransa walikuwa wakitaka Waalgeria wapeleke balozi wao nchini Ufaransa kwa ajili ya kusuluhisha suala hilo.
Wakati anakwenda balozi huyo alienda na zana za kijeshi zikielekezwa kwenye mojawapo ya meli za Kifaransa, ndipo Wafaransa wakaona kuna haja ya kutumia nguvu dhidi ya watu hao.
Deval na wakazi wengine wa Ufaransa waliondoka Algiers na kurudi zao Ufaransa wakati Waziri wa Vita Clermont-Tonnerre alipendekeza hatua za kijeshi zichukuliwe na majeshi yaaanze kwenda huko.
Hatua hiyo haikuungwa mkono na baadhi ya watu wa Ikulu wakikataa matumizi ya nguvu za kijeshi. Kamanda wa Kijeshi Admiral Duperré aliamuru meli za kijeshi 600 huko Toulon kujiandaa na kazi huko Algiers.
Akitumia mpango wa Napoleon 1808 kwa ajili ya kuivamia Algeria, Jenerali Bourmont alilikamata eneo la kilometa 27 magharibi mwa Algiers huko Sidi Ferruch.
Waalgeria hawakukaa kimya waliamua kujibu mapigo kwa kupanga wanajeshi wa 7,000 Kisultan pia wanajeshi wengine 19,000 kutoka majimbo ya Constantine na Oran (Uturuki), wenyeji asilia wa Kiberiberi 17,000 walijipanga kupambana na uonevu huo.
Julai 5 majeshi ya Ufaransa yalibisha hodi katika jiji la Algiers na baada ya majuma matatu ya mapambano wenyeji wa Algeria walikubali kujisalimisha kwa makubaliano maalum ikiwamo kurudishiwa utajiri wao.
Hivyo basi ujio wa kijeshi wa Wafaransa katika ardhi hiyo ulimaliza kabisa utawala wa dola la Ottoman katika eneo hilo kwani majeshi yake yaliondoka kwenda barani Asia.
0 Comments:
Post a Comment