Kanisa la Assembles Of God
(TAG), Amani Soweto la mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, linatarajia kufanya
maombi ya shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa namna anavyoendelea kuwalinda na
kuwaepusha Watanzania dhidi ya madhara yanayotokanayo na janga la Covid- 19
Aidha maombi hayo yataenda
sanjari na maombi ya kumshukuru Mungu kwa
kuweza kumaliza nusu mwaka huku wakimuomba Mungu aweza kuwafikisha
katika nusu mwaka mwingine tena.
Akizungumza na Waandishi wa
habari ofisini kwake Askofu Mkuu Mkuu wa Jimbo la Kilimanjaro Magharibi Dkt.
Benjamin William Bukuku, alisema kanisa la TAG Amani Soweto limendaa maombi
maalum ya shukrani yatakayo fanyika Juni 28 mwaka huu kanisa hapo.
“Tunapomaliza miezi sita ya
mwaka, TAG tumeona mambo makubwa ambayo Mungu amezidi kututendea licha ya janga
la virusi vya ugonjwa wa Corana kutokea, lakini sisi kama Watanzania ameweza
kutuokoa,”alisema Askofu Dkt. Bukuku.
Dkt. Bukuku alisema baada
ya kauli ya Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli ya kuwataka Watanzani kwa imani zao kumshukuru Mungu kwa kuliepusha
taifa na janga la Corona imesaidia kuwaondolea hofu Watanzania.
Askofu Bukuku ambaye pia ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Amani Soweto
alisema ugonjwa Covid-19 ulikuja ghafla
na kuzua hofu kubwa miongoni wa watu wengi
na nchini nyingi duniani ikiwemo Tanzania.
Alisema katika maombi hayo
yataongozwa na Askofu wa Kanisa la Assembles Of God (TAG), Jimbo Kuu la Kiteto
Askofu Efatha Simon, ambaye atakuwa mgeni rasmi katika maombi hayo huku mgeni
rasmi katika maombi hayo atakuwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira.
0 Comments:
Post a Comment