Mama Minde ni jina ambalo unapopita katika viunga vya mkoa
wa Kilimanjaro kutoka Same hadi Hai sio geni kabisa. Wakazi wa maeneo
hayo hakika wanamfahamu sana mwanamke huyu.
Ukimuuliza mtu Je, unamfahamu Elizabeth Minde atakwambia
“…aaah! Huyu mama Minde, mwanasheria na mama wa KWIECO?,” Kila mtu aliyekaa
katika mkoa wa Kilimanjaro kwa zaidi ya miaka mitano atakwambia mwanamke huyu
ni mwanamke mwenye sifa zipi.
Leo tutamwangazia mwanamke huyo miongoni mwa wengi wenye
shauku ya kuwa viongozi katika jamii ambaye mni Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya
kiserikali iliyoanzishwa mwaka 1987 yenye malengo ya kulinda na kutetea haki za
jamii hususani Wanawake mkoani Kilimanjaro (KWIECO).
UONGOZI NI KIPAJI AU MAFUNZO
Kwa mtazamo wake Mama Minde ana tafsiri “Uongozi” ni
kusaidia kutoa dira au kuwa na uthubutu hata kama mifumo hairuhusu.
Mwanamke huyo anaamini kuwa kuthubutu ndio chachu ya
kuwaleta wanawake kuanza kuwania nafasi mablimbali za uongozi.
Mama Minde anasema kila binadamu ana kipaji chake lakini
kipaji bila mafunzo kinakuwa kazi bure akimaanisha bila kukipalilia kwa kukipa
elimu.
“Binafsi nilibahatika kusomeshwa labda wenzangu hawakupata
fursa hiyo, lakini elimu ndio jambo la kwanza kuimarisha uwezo wa mtu,” anasema
Minde.
Aidha Mama Minde anasema yeye alikuwa kiongozi kutoka
anazaliwa lakini bado alikwenda kusoma ili kuongeza uelewa wa masuala
mbalimbali, kwani yeyote anayetaka kuwa kiongozi sharti awe na uelewa mpana ili
kuondoa mkanganyiko pindi atakapopata nafasi ya kuiongoza jamii.
“Nimekuwa kiongozi tangu shule ya msingi, nilikuwa
kiongozi wa kidini, sekondari pia na Chuoni pale Dar es Salam nilikuwa
mwakilishi wa wanafunzi katika serikali ya wanafunzi,” anasema Mama Minde.
“Nilisomea sheria, ndoto yangu tangu nikiwa mdogo ilikuwa
ni ualimu hata walimu wangu walinitaka nikausomee ualimu hata hivyo siku moja
Mwalimu Mkuu aliniuliza unapenda nini nikasema sheria, mwalimu aliniongoza
nikajaze kwa ajili ya kwenda kujiunga chuo kikuu,” anasema Mama Minde.
“Labda nafikiri bado wito ulikuwamo ndani ndio sababu
nimekuwa mwanaharakati wa masuala ya wanawake kupitia KWIECO ambako mara zote
tumekuwa tukijita kuelemisha wanawake kujitambua kuhusu umuhimu wao,”
anaongeza.
ILIKUWAJE ALIPOTUA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
“Miaka ile ya 1970 kumuona mwanamke anasomea sheria
lilikuwa ni jambo la kushangaza mno, wakati naingia UDSM kwanza tulikuwa 40
darasa zima hala cha kuogofya ni kwamba wanawake tulikuwa watano tu, wawili
walikuwa wakenya, na watatu ndio watanzania,” anasema Mama Minde.
Haikuishia hapo Mama Minde anasema baadhi ya walimu nao
walikuwa na mtazamo hasi kuhusu wanafunzi wa kike kusomea sheria chuoni hapo.
“Changamoto zikaanzia hapo pia kwani baadhi ya walimu nao
walikuwa wakituonaje sijui, vitivo vingine pale pale chuoni walikuwa
wakitutazama kwa jicho baya utafikiri tumeua,” anasema mwanamke huyo.
“Masomo ya Development Studies tuliyokuwa tukisoma pale
chuoni chuo kizima ndio yalianza kutufikirishakuwa jamii yetu ni jamii ya namna
gani,” anaongeza Mama Minde.
“Kwenda chuoni kulinijenga sana kifikra na hapo ndipo
nikawa nawaza tunawasaidiaje wanawake wenzetu kujikwamua kutoka hapa tulipo
kwenda katika nafasi nyingine,” anasema Mama Minde.
Baada ya hapo alikwenda kufundisha katika Chuo Kikuu cha
Ushirika mjini Moshi (MUCCOBs), ambako huko nako alikutana changamoto kwani
wengi walikuwa wakimwangalia kwanini wafundishwe na mwanamke hali ambayo
hawakuwa na namna lakini kuna wakati ilikuwa kikwazo.
NINI KIFANYIKE KUMWEZESHA MWANAMKE
Mama Minde anasema wanawake wenyewe wanapaswa kuondoka na
hofu ili kujijengea uaminifu hali ambayo itaimarisha uthubutu.
“Mwanamke ni mfanyakazi wa mambo makubwa, changamoto ni
kwamba hata takwimu za taifa hazisemi mambo makubwa ambayo mwanamke
anayafanya,” anasema Mama Minde
Aidha Mama Minde anasema mwanamke anatakiwa kujitambua na
kuthamini badala ya kusubiri kupigiwa kelele
“Dhana ya mwanamke kuitwa mama wa nyumba hiyo dhana
inatakiwa iondoke na mwanamke mwenyewe anatakiwa kuwa kwanza kuondoka na dhana
hiyo.”
Pia Mama Minde anasema wanawake wengi wa kitanzania
hawapendi kujielimisha jambo ambalo linawaweka mahali pagumu, hata hivyo
alisisitiza kuwa kujielimisha sio lazima mtu aingie darasani isipokuwa kitu
ambacho mtu anaelewa anapokuwa na uwezo wa kumwelezea mtu mwingine na huyo mtu
akikaa na kutafakari aweze kumwelewa huko ndiko kujielimisha.
Mama Minde alikeme mfumo dume ambao alimtaja mwanamke kama
ndiye Mwalimu Mkuu wa Mfumo Dume jambo ambalo limekuwa likichangia kwa kiasi
kikubwa kuchelewa kupata viongozi wanawake wenye utashi.
“Tangu mtoto anazaliwa anakuzwa na huyo mama, akitegemea
kauli kuu kutoka kwa mumewe sasa mtoto akiwa mtu mzima anakuwa katika mfumo ule
ule ambao sio rafiki, elimu kandamizi lazima ikarabatiwe ili kumtengeneza
mwanamke tangu akiwa mtoto,” anasema Mama Minde.
MATARAJIO YAKE
Licha ya changamoto zilizopo katika mfumo wa sera,
miongozi, kanuni katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Minde
anao kuna umuhimu wa kuendelea kupigania haki na usawa kwa mwanamke dhidi ya
ukandamizaji unafanywa hadi pale mambo yatakapokuwa sawa.
“Ushawishi na utetezi katika sera na kanuni katika
nchi yetu bado ni changamoto, tumekuwa tukiungana kupaza sauti kwa ajili ya
mwanamke lakini sio kazi ya siku moja, hivyo uelemishaji ndio kazi ya msingi
katika masuala haya kumfanya mwanamke ajitambue,”
Pia Mama Minde anaapa hatajakata tamaa hata kidogo katika
kuwania uongozi kwani hata sasa amefanikiwa pakubwa kwani katika Chama cha
Mapinduzi (CCM) bado ana nafasi ya kufanya vizuri zaidi huku akisisitiza
wanawake wenzake wasikate tama
“Mwanamke ni rahisi sana kukata tama utasikia eti
tumuachie Mungu, kwa kweli kwa mtazamo huo hatuwezi kutoka mahali tulipo kwanza
hata huyo Mungu wa wanawake atakuwa amechoka kusikiliza maneno hayo,” anasema
Mama Minde.
Mnamo mwaka 2010 waliingia katika kinyang’anyiro cha
kuwania ubunge ndani ya chama ambapo wanawake walikuwa wawili na Zakia Meghji
lakini akapita yeye licha ya kushindwa kuchaguliwa na wananchi wa Jimbo la
Moshi Mjini. Mnamo mwaka 2015 alipambana tena na kupita yeye mwenyewe ndani ya
chama lakini bado hakufanikiwa kupata nafasi ya kupigiwa kura na wananchi.
Elizabeth Minde alizaliwa Oktoba 19, 1948 huko Kirara, Old
Moshi katika mkoa wa Kilimanjaro. Ana watoto watatu wawili wa kiume na mmoja wa
kike.
Mama Minde ni jina ambalo unapopita katika viunga vya mkoa
wa Kilimanjaro kutoka Same hadi Hai sio geni kabisa. Wakazi wa maeneo
hayo hakika wanamfahamu sana mwanamke huyu.
Ukimuuliza mtu Je, unamfahamu Elizabeth Minde atakwambia
“…aaah! Huyu mama Minde, mwanasheria na mama wa KWIECO?,” Kila mtu aliyekaa katika
mkoa wa Kilimanjaro kwa zaidi ya miaka mitano atakwambia mwanamke huyu ni
mwanamke mwenye sifa zipi.
Leo tutamwangazia mwanamke huyo miongoni mwa wengi wenye
shauku ya kuwa viongozi katika jamii ambaye mni Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya
kiserikali iliyoanzishwa mwaka 1987 yenye malengo ya kulinda na kutetea haki za
jamii hususani Wanawake mkoani Kilimanjaro (KWIECO).
UONGOZI NI KIPAJI AU MAFUNZO
Kwa mtazamo wake Mama Minde ana tafsiri “Uongozi” ni
kusaidia kutoa dira au kuwa na uthubutu hata kama mifumo hairuhusu.
Mwanamke huyo anaamini kuwa kuthubutu ndio chachu ya
kuwaleta wanawake kuanza kuwania nafasi mablimbali za uongozi.
Mama Minde anasema kila binadamu ana kipaji chake lakini
kipaji bila mafunzo kinakuwa kazi bure akimaanisha bila kukipalilia kwa kukipa
elimu.
“Binafsi nilibahatika kusomeshwa labda wenzangu hawakupata
fursa hiyo, lakini elimu ndio jambo la kwanza kuimarisha uwezo wa mtu,” anasema
Minde.
Aidha Mama Minde anasema yeye alikuwa kiongozi kutoka
anazaliwa lakini bado alikwenda kusoma ili kuongeza uelewa wa masuala
mbalimbali, kwani yeyote anayetaka kuwa kiongozi sharti awe na uelewa mpana ili
kuondoa mkanganyiko pindi atakapopata nafasi ya kuiongoza jamii.
“Nimekuwa kiongozi tangu shule ya msingi, nilikuwa
kiongozi wa kidini, sekondari pia na Chuoni pale Dar es Salam nilikuwa
mwakilishi wa wanafunzi katika serikali ya wanafunzi,” anasema Mama Minde.
“Nilisomea sheria, ndoto yangu tangu nikiwa mdogo ilikuwa
ni ualimu hata walimu wangu walinitaka nikausomee ualimu hata hivyo siku moja
Mwalimu Mkuu aliniuliza unapenda nini nikasema sheria, mwalimu aliniongoza
nikajaze kwa ajili ya kwenda kujiunga chuo kikuu,” anasema Mama Minde.
“Labda nafikiri bado wito ulikuwamo ndani ndio sababu
nimekuwa mwanaharakati wa masuala ya wanawake kupitia KWIECO ambako mara zote
tumekuwa tukijita kuelemisha wanawake kujitambua kuhusu umuhimu wao,”
anaongeza.
ILIKUWAJE ALIPOTUA CHUO KIKUU
CHA DAR ES SALAAM
“Miaka ile ya 1970 kumuona mwanamke anasomea sheria
lilikuwa ni jambo la kushangaza mno, wakati naingia UDSM kwanza tulikuwa 40
darasa zima hala cha kuogofya ni kwamba wanawake tulikuwa watano tu, wawili
walikuwa wakenya, na watatu ndio watanzania,” anasema Mama Minde.
Haikuishia hapo Mama Minde anasema baadhi ya walimu nao
walikuwa na mtazamo hasi kuhusu wanafunzi wa kike kusomea sheria chuoni hapo.
“Changamoto zikaanzia hapo pia kwani baadhi ya walimu nao
walikuwa wakituonaje sijui, vitivo vingine pale pale chuoni walikuwa
wakitutazama kwa jicho baya utafikiri tumeua,” anasema mwanamke huyo.
“Masomo ya Development Studies tuliyokuwa tukisoma pale
chuoni chuo kizima ndio yalianza kutufikirishakuwa jamii yetu ni jamii ya namna
gani,” anaongeza Mama Minde.
“Kwenda chuoni kulinijenga sana kifikra na hapo ndipo
nikawa nawaza tunawasaidiaje wanawake wenzetu kujikwamua kutoka hapa tulipo
kwenda katika nafasi nyingine,” anasema Mama Minde.
Baada ya hapo alikwenda kufundisha katika Chuo Kikuu cha
Ushirika mjini Moshi (MUCCOBs), ambako huko nako alikutana changamoto kwani
wengi walikuwa wakimwangalia kwanini wafundishwe na mwanamke hali ambayo
hawakuwa na namna lakini kuna wakati ilikuwa kikwazo.
NINI KIFANYIKE KUMWEZESHA
MWANAMKE
Mama Minde anasema wanawake wenyewe wanapaswa kuondoka na
hofu ili kujijengea uaminifu hali ambayo itaimarisha uthubutu.
“Mwanamke ni mfanyakazi wa mambo makubwa, changamoto ni
kwamba hata takwimu za taifa hazisemi mambo makubwa ambayo mwanamke
anayafanya,” anasema Mama Minde
Aidha Mama Minde anasema mwanamke anatakiwa kujitambua na
kuthamini badala ya kusubiri kupigiwa kelele
“Dhana ya mwanamke kuitwa mama wa nyumba hiyo dhana
inatakiwa iondoke na mwanamke mwenyewe anatakiwa kuwa kwanza kuondoka na dhana
hiyo.”
Pia Mama Minde anasema wanawake wengi wa kitanzania
hawapendi kujielimisha jambo ambalo linawaweka mahali pagumu, hata hivyo
alisisitiza kuwa kujielimisha sio lazima mtu aingie darasani isipokuwa kitu
ambacho mtu anaelewa anapokuwa na uwezo wa kumwelezea mtu mwingine na huyo mtu
akikaa na kutafakari aweze kumwelewa huko ndiko kujielimisha.
Mama Minde alikeme mfumo dume ambao alimtaja mwanamke kama
ndiye Mwalimu Mkuu wa Mfumo Dume jambo ambalo limekuwa likichangia kwa kiasi
kikubwa kuchelewa kupata viongozi wanawake wenye utashi.
“Tangu mtoto anazaliwa anakuzwa na huyo mama, akitegemea
kauli kuu kutoka kwa mumewe sasa mtoto akiwa mtu mzima anakuwa katika mfumo ule
ule ambao sio rafiki, elimu kandamizi lazima ikarabatiwe ili kumtengeneza
mwanamke tangu akiwa mtoto,” anasema Mama Minde.
MATARAJIO YAKE
Licha ya changamoto zilizopo katika mfumo wa sera,
miongozi, kanuni katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Minde
anao kuna umuhimu wa kuendelea kupigania haki na usawa kwa mwanamke dhidi ya
ukandamizaji unafanywa hadi pale mambo yatakapokuwa sawa.
“Ushawishi na utetezi katika sera na kanuni katika
nchi yetu bado ni changamoto, tumekuwa tukiungana kupaza sauti kwa ajili ya
mwanamke lakini sio kazi ya siku moja, hivyo uelemishaji ndio kazi ya msingi
katika masuala haya kumfanya mwanamke ajitambue,”
Pia Mama Minde anaapa hatajakata tamaa hata kidogo katika
kuwania uongozi kwani hata sasa amefanikiwa pakubwa kwani katika Chama cha
Mapinduzi (CCM) bado ana nafasi ya kufanya vizuri zaidi huku akisisitiza
wanawake wenzake wasikate tama
“Mwanamke ni rahisi sana kukata tama utasikia eti
tumuachie Mungu, kwa kweli kwa mtazamo huo hatuwezi kutoka mahali tulipo kwanza
hata huyo Mungu wa wanawake atakuwa amechoka kusikiliza maneno hayo,” anasema
Mama Minde.
Mnamo mwaka 2010 waliingia katika kinyang’anyiro cha
kuwania ubunge ndani ya chama ambapo wanawake walikuwa wawili na Zakia Meghji
lakini akapita yeye licha ya kushindwa kuchaguliwa na wananchi wa Jimbo la
Moshi Mjini. Mnamo mwaka 2015 alipambana tena na kupita yeye mwenyewe ndani ya
chama lakini bado hakufanikiwa kupata nafasi ya kupigiwa kura na wananchi.
Elizabeth Minde alizaliwa Oktoba 19, 1948 huko Kirara, Old
Moshi katika mkoa wa Kilimanjaro. Ana watoto watatu wawili wa kiume na mmoja wa
kike.
0 Comments:
Post a Comment