Monday, June 15, 2020

Kukua kwa kundi la chuki la Ku Klux Klan (KKK)

Juni 15, 1927  Kundi la ubaguzi wa rangi nchini Marekani la Ku Klux Klan (KKK) lilianza kukua kwa kasi katika majimbo ya Kusini ya Marekani huku likizidisha visa vya kuwanyanyasa Wamarekani weusi. 

Mojawapo ya ukatili kundi hili ilikuwa ni kuwapiga na kuwatesa wanawake na watoto. Kwa upande wa kaskazini Wamarekani weusi waliokuwapo huku walikuwa wakidai kundi hili lifutwe. 

Mojawapo ya kisa kilicholikuza kundi hili ni kile kilichotokea Gainsville huko Georgia ambako mwanamke mmoja na mtoto wake wa kiume walitolewa kwenye kitanda chao kisha kutolewa mjini humo kwa kipigo bila kosa lolote. 

Pia waathirika hao Wamarekani weusi walitakiwa kuondoka eneo hilo mara moja na wakikataa mabaya zaidi yangewapata. Mwanamke huyo  alipofikishwa hospitalini alikutwa na alama 82 za viboko katika sehemu mbalimbali za mwili.
KKK lilikuwa ni kundi la chuki lililoundwa na Wamarekani weupe  ambao malengo yake ilikuwa ni kuzuia Wamarekani wenye asili ya Afrika kuongezekana na kuchukua ardhi hiyo na rasimali zake. 

Kundi hili limekuwa katika maeneo matatu katika historia ya Marekani. Kila mmoja ametetea msimamo mkali wa athari kama utaifa mweupe, kupinga uhamiaji na Ukatoliki. Lilianza kwa mara ya kwanza mwaka 1865–1871, mara ya pili ilikuwa 1915–1944 na mara ya tatu 1946 hadi sasa. 

Ukuaji wa kundi hili katikati ya miaka ya 1920 ulionekana kutokana idadi kubwa ya wanachama wake kutoka milioni tatu hadi milioni sita. Lakini kwa sasa lina wanachama kati ya 5,000 hadi 8,000.

0 Comments:

Post a Comment