Juni 18, 1925 alifariki dunia mwanasiasa wa Marekani Robert Mario La Follete Sr. Alikuwa akifahamika sana kwa jina la Fighting Bob.
Ni msomi wa masuala ya sheria na mwanasiasa ambaye anakumbukwa kama mwanzilishi wa Chama cha Progressive ambapo mnamo mwaka 1924 aliingia katika kinyang'anyiro cha Urais wa taifa hilo.
Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 70 jijini Washington D.C kwa maradhi ya moyo.
Alizikwa kwatika makaburi ya Forest Hill karibu kabisa upande wa Magharibi wa Madison huko Wisconsin.
La Follete aliwahi kuhudumu katika nafasi ya Ugavana wa Wisconsin na pia katika Chambers of Congress.
Siasa zake zilikuwa za mrengo wa Republican katika maisha yake nchini Marekani hata kabla ya kuanzisha chama chake.
Mwanahistoria John D. Buenker aliwahi kumwelezea La Follete Sr kuwa ni mtu ambaye anaadhimishwa zaidi katika historia ya Wisconsin. La Follete alishinda mara mbili uchaguzi wa mwaka 1902 na 1904 lakini mwaka 1905 bunge lilimchagua kuwa seneta wa Marekani.
Aliibukia huko kama kiongozi wa kitaifa wa Progressive baada ya kupambana vikali na Nelson Aldrich.
Awali alikuwa akiimuunga mkono Rais William Howard Taft lakini ushirika wao ulikoma baada ya Taft kushindwa kushinikiza kupunguzwa kwa viwango vya kodi nchini humo.
La Follete alitoa upinzani mkali katika kuwania nafasi ya kuteuliwa kuwa Rais ndani ya chama cha Republican mnamo mwaka 1912 lakini uteuzi wake ulifunikwa na Rais wa zamani Theodore Roosevelt.
Katika uchaguzi wa mwaka 1924 kwa tiketi ya chama cha Progressive La Follete alishinda kwa 16.6% ya kura ikiwa ni ushindi mzuri kwa chama nje ya Democratic na Republican.
Alifariki dunia muda mfupi baada ya uchaguzi huo kufanyika na wanawe wa kiume Robert M. La Follette Jr. na Philip La Follette, walikalia kuongoza chama cha Progressive huko Wisconsin.
0 Comments:
Post a Comment