Picha maarufu ya Mauaji wa Soweto ilipigwa na
mwandishi wa habari Sam Nzima ambaye kwa sasa hatunaye ulimwenguni alifariki
dunia mnamo Mei 12, 2018 katika Hospitali ya Rob Ferreira, Nelspruit, nchini
Afrika Kusini akiwa na miaka 84. Picha hiyo imekuwa ikifahamika kwa jina la ‘Hector
Pietersen’.
Story ya mtoto huyo inaanza
hivi; Jina lake halisi mtoto huyo ni Zolile Hector Pietersen. Hata hivyo jina halisi
la ukoo wake ni Pitso, lakini familia hiyo ililazimika kubadili na kuwa
Pietersen ili kuendana na falsafa ya ubaguzi wa rangi nchini humo, na kujihisi
kama wao ni makaburu ilhali wakiwa ni weusi. Familia hiyo iliamua kufanya hivyo
ili kukwepa dhuluma za makaburu. Hata jina la Zolile lilifutwa kwa muda ili
apate nafasi ya kusoma.
Zolile alizaliwa Agosti 19,1963
mjini Soweto nchini Afrika Kusini wakati falsafa ya ubaguzi wa rangi ikiwa
imepamba moto. Falsafa ya ubaguzi wa rangi ilikuwa ikijulikana kama Apartheid,
ambayo ilikuwa ikiendeshwa na makaburu waliokuwa wakitawala nchi ya Afrika
Kusini.
Zolile alikuwa akihudhuria
shuleni kwa taabu hasa alipokuwa akipita sehemu mbalimbali ili kuelekea
shuleni. Alipita kwa wasiwasi mkubwa akiwa na hofu ya kufyatuliwa risasi.
Baadae alizoea hali ya milio ya risasi mara kwa mara katika mji wa Soweto.
Alikuwa akienda shuleni
mara nyingi akiambatana na dada yake Antoinete Sithole pamoja na rafiki yao
kipenzi Mbuyisa Makhubo. Mbuyisa Makhubo alimtangulia Zolile Hector Pietersen
miaka mitano kuzaliwa, hivyo alimchukulia kama kaka yake. Watatu hao walikuwa
na furaha wanapokutana na kuzungumza pamoja na vilevile wakati wa shida
hawakukosa kuwa pamoja ilipobidi.
Serikali ya Makaburu nchini
Afrika Kusini iliweka utaratibu wa 50/50 katika mitaala yote hasa katika elimu
ya msingi na sekondari. Kulikuwa na masomo muhimu zaidi ambayo yalikuwa
yakifundishwa kwa lugha ya kiingereza, na yale ambayo hayakuwa na umuhimu sana
yalikuwa yakifundishwa katika lugha ya Kiafrikaan. Na mitihani ilikuwa
ikitolewa kulingana na lugha husika inayotumika kufundishia katika somo husika.
Mnamo Juni 16, 1976, Zolile,
Antoinete Sithole pamoja na rafiki yao kipenzi Mbuyisa o walipokuwa shuleni
wakihudhuria masomo walifikwa na wakati mgumu walipoanza kugoma kufundishwa
masomo kwa lugha ya Kiingereza badala ya lugha yao mama ya Kiafrikaan. Ndipo
polisi wa makaburu walipoanza vurugu ya kuwashambulia wanafunzi pamoja na watu
wengine.
Wanafunzi walikusanyika
pamoja kwa amani na kueleza kile walichokuwa wakikipinga katika taaluma. Muda
mfupi baadae, mkusanyiko wa wanafunzi hao wakiwemo Zolile, Antoinete na Mbuyisa,
ulishambuliwa mara tu polisi walipowasili shuleni hapo. Ndipo wanafunzi hao
walianza kuokota mawe na kuwarushia polisi wa makaburu waliofika kuwatawanya
kwa risasi.
Mkusanyiko wa wanafunzi hao
ulikuwa na wanafunzi yapata 13,000 pamoja na wafanyakazi weusi wa shule hiyo
ambapo katika wafanyakazi wa shule hiyo, wawili waliuawa kwa kupigwa risasi na
polisi wa Makaburu. Kwa ghadhabu, wanafunzi waliongeza fujo ili kutetea haki ya
kitaaluma waliyokuwa wakiidai na vilevile kulinda utu wao. Walichoma magari
kadhaa moto na majengo. Pia walilishambulia jengo la kiengo cha Elimu mkoa wa
Transvaal.
Wanafunzi 30 walikusanyika
nje ya shule ya sekondari ya Phefeni wakiwa wanaimba wimbo mkuu wa Kisotho.
Polisi walipowasili katika shule hiyo, mkusanyiko huo nao ulishambuliwa na
polisi hao ambapo wanafunzi nao walikuwa wakiwarushia mawe polisi.
Polisi walifyatua mabomu ya
gesi inayoumiza macho na kutoa machozi kwa wanafunzi hao. Haijulikani nani
alitoa amri ya kutumika kwa risasi za moto kuwafyatulia mkusanyiko ule wa
wanafunzi. Wanafunzi hao walianza kukimbia na kutawanyika ovyo ili kuokoa
maisha yao. Wengine walikuwa wakigaragara barabarani wakilalamika maumivu baada
ya kupigwa risasi.
Zolile aliripotiwa kuwa
mwanafunzi wa kwanza kufariki baada ya kuwasili katika zahanati akiwa na
majeraha ya risasi.
Lakini pia mwanafunzi
Hasting Ndlovu aliripotiwa kufariki kutokana na majeraha ya risasi alizopigwa
na polisi wa Makaburu. Lakini kutokana na kutokuwepo kwa picha iliyopigwa ya
Hastings Ndlovu, imehesabiwa kuwa mwanafunzi aliyewapa simanzi watu wengi
nchini Afrika kusini ni Zolile.
Zolile alipigwa risasi
akiwa na dada yake pamoja na rafiki yao kipenzi Mbuyisa Makhubo, alidondokea
katika kona ya nyumba moja mpakani mwa mtaa wa Moema na mataa wa Vilakazi; Mbuyisa
Makhubo alimnyanyua Zolile akiwa na dada yake Antoinete Sithole.
0 Comments:
Post a Comment