Monday, June 15, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Choi Hong Hi ni nani?

Juni 15, 2002 alifariki mwanamichezo anayechukuliwa kuwa ni mwanzilishi wa sanaa ya mapigano ya Taekwondo (Taekwon-Do) Choi Hong Hi. 

Huyu alikuwa Jenerali wa Jeshi la Korea Kusini na mpiganaji wa sanaa za mapigano huku akiacha nembo ya kuwa mtata katika sanaa hiyo nchini Korea. 

Choi Hong Hi alifariki dunia jijini Pyongyang huko Korea Kaskazini. Alizaliwa Novemba 9, 1918 katika kitongoji cha Hwa Dae Myongchon, Korea Kaskazini wakati huo ikishikiliwa na Japan.
 
Choi alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 83 kwa maradhi ya saratani. Alipewa heshima ya kitaifa na kuzikwa katika viunga ambako Mashujaa Wazalendo wa Korea huzikwa huko Sinmi-dong. 
Choi aliingizwa katika Jumba la Wakongwe waTaekwondo akiwa na majina mengi. Anatajwa kama "Baba wa Taekwon-Do," "Mwanzilishi na Rais wa kwanza wa Shirikisho la Kimataifa la Taekwon-Do ," na "Mwanzilishi wa Oh Do Kwan." 

Wakati anafariki alimwacha mkewe Choi Joon Hee, mtoto wa kiume Choi Jung Hwa na mabinti zake wawili Sunny na Meeyun na pia wajukuu. 

Choi alilazimishwa kuhudumu katika Majeshi ya Japan katika Vita vya Pili vya Dunia lakini wakati akiwa huko alijikuta katika wakati mgumu ambao ulimfanya atupwe jela kutokana na kufanya mazoezi ya sanaa ya mapigano. 

Kutokana na vita Januari 1946 Choi alipanda cheo na kutunukiwa Luteni wa Pili wa Jeshi la Korea. 
Kutoka mwaka 1946 hadi 1951 Choi alitunukiwa kuwa Luteni wa kwanza, captain, Meja, Luteni Kanali, Kanali na kisha Brigedia Jenerali. Alipata kuwa Meja Jenerali mnamo mwaka 1954.

0 Comments:

Post a Comment