Juni 25, 2009 alifariki mfalme wa Pop raia wa Marekani
Michael Jackson. Jackson alifariki dunia mwaka 2009 akiwa na miaka 50 kutokana
na kuzidisha madawa. Alizikwa huko Forest Lawn Memorial Park, Glendale jimboni California.
Michael Jackson alizaliwa Agosti 29, 1958, huko Gary
katika Jimbo la Indiana. Jackson alikuwa ni mtoto wa nane kati ya kumi wa Mzee Joe
Jackson na Catherine Jackson, alikuwa na dada zake watatu ambao ni Rebbie, La Toya na Janet, pia kaka
zake ni Jackie, Tito, Jermaine, Marlon, Randy, na ndugu yake mwingine anayeitwa
Brandon alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Alianza kuimba akiwa umri wa miaka mitano akiwa na
kundi la Jackson 5, kundi la kifamilia kwani waimbaji wote katika kundi hilo
walikuwa ni ndugu zake wa damu, kundi hilo lilifanya vizuri sana nchini Marekani
na dunia nzima kwa ujumla.
Jackson hakuwa na mahusiano mazuri na baba yake aliwahi
kusema kuwa alikuwa na kawaida ya kumchapa Michael wakati akiwa mtoto, na
Michael aliwahi kulalamika kuwa baba yake alikuwa akimnyanyasa kwa kumpiga hasa
wakati wa mazoezi ingawa aliwahi kukiri kuwa baba yake alichangia kwa kiasi
kikubwa yeye kupata mafanikio.
Mnamo mwaka 1968 Boby Taylor na The Vancouver
waliligundua Kundi la Jackson 5 ambapo kundi hilo liliingia mkataba na Motown
Records na walifanikiwa kurekodi nyimbo zilizotisha enzi hizo kama ABC, I Want u
Back, I’ll be there na nyinginezo, walirekodi albamu 14 na Motown na Michael
alirekodi albamu nne za solo.
Jackson 5 walikaa na Motown mpaka ilipofika mwaka 1976
ambapo walidai wanataka uhuru wa kisanii na baada ya hapo wakaenda kusign na
Epic, na kundi hilo lilibadilisha jina kutoka The Jackson 5 na kujiita The
Jacksons na walirekodi albamu sita kati ya mwaka 1976 hadi 1984.
Mnamo mwaka 1977 Michael Jackson alikutana na
mtaarishaji wa muziki maarufu enzi hizo Quincy Jones chini ya Epic Records
akarekodi albamu inayoitwa Off the Wall, ambayo ilifanya vizuri katika chart za
nchi Marekani.
Mnamo 1982 Wacko Jacko aliachia albamu ambayo ambayo
iliuza sana kuliko album yoyote duniani, inaitwa Thriller, ndani ya albamu hii
kulikuwa na Single 7 ambazo ziligonga vichwa vya watu sana dunia nzima, zaidi ya
copy milioni 50 ziliuzwa, alifanya kazi na waandaji bora na waongozaji wazuri kufanikiwa
kutengeneza Music video ya Thriller ambayo mpaka leo bajeti ya kutengeneza
music video hiyo bado ni gumzo.
Ilipofika 1984 Jackson alivunja rekodi kwa kutunukiwa
tuzo 8 za grammy ndani ya usiku mmoja, tuzo hizo zilitokana na Albamu yake ya
Thriller na kitabu cha “T story book.” Desemba 9, 1984 katika concert ya mwisho
ya Jackson 5 iliyoitwa Jackson Victory Tour, Wacko Jacko akatangaza kuwa
anajitoa kutoka kundi hilo na atakuwa anafanya kazi zake binafsi.
Mnamo mwaka 1987 Michael Jackson akaachia albamu yake
iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wake album inaitwa BAD na kuvunja
rekodi ya Tour za msanii mmoja mmoja yaani Solo, kwani show zake zilikuwa
zikihudhuriwa na maelfu ya watu kila nchi aliyokanyaga.
0 Comments:
Post a Comment