Juni 5, 2004 alifariki dunia Rais wa 40 wa Marekani Ronald
Reagan. Reagan aliitawala Marekani kutoka mwaka 1981 hadi mwaka 1989. Alichukua
mikoba ya Jimmy Carter. Reagan alikuwa mpenda michezo tangu kuzaliwa kwake.
Mnamo Agosti 1994 akiwa na umri wa miaka 83 iliripotiwa kuwa
Reagan ameathirika na ugonjwa wa Alzhemeir ambao huanza kwa mtu kushindwa kukumbuka
matukio ya sasa hivi. Hata hivyo aliendelea kuishi na hali hiyo hadi mchana wa
Juni 5, 2004 alipopatwa naa kichomi kilichosababishwa na maradhi hayo ya
Alzhemeir na kufariki dunia. Mkewe Nancy (1921-2016) alithibitisha kutokea kwa
kifo hicho. Reagan alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 93 na miaka 12
alifariki mkewe huyo akiwa na umri wa miaka 94.
Akiwa jijini Paris Rais wa 41 wa Marekani George H. W Bush alitangaza
kuwa Juni 11 itakuwa siku maalumu ya maombolezo kutokana na kifo vha kiongozi
huyo aliyefanya naye kazi akiwa makamu wa Rais. Mwili wake ulichukuliwa hadi Santa
Monica huko California na kuzikwa katika Makataba ya Kumbukumbu za Rais Ronald
Reagan (Ronald Reagan Presidential Library)
Rais huyo zamani wa Marekani aliwaita tumbili wajumbe wa
Afrika katika Umoja wa Mataifa UN mwaka 1971 wakati alipokuwa gavana wa Jimbo
la California katika ukanda wa sauti uliochapishwa na The Atlantic. Alitoa
matamshi hayo ya kibaguzi katika mawasiliano ya simu kwa aliyekuwa wakati huo
rais wa Marekani Richard Nixon ambaye alirekodi simu zake zote.
Reagan alikasirishwa kwamba wajumbe wa Afrika katika Umoja wa
Mataifa UN hawakuiunga mkono Marekani katika kura ya kuitambua China na kuipiga
marufuku Taiwan. Reagan alisema, Kuwaona hao 'tumbili' kutoka mataifa ya
Afrika, bado hawafurahii kuvaa viatu! Matamshi hayo yalimfanya Nixon kucheka. Sauti
hiyo ilifichuliwa na Tim Naftali, Profesa wa Historia katika chuo kikuu cha New
York, ambaye alikuwa mwelekezi katika maktaba ya rais Nixon ambayo ilihifadhi
kanda zote zilizorekodiwa za rais huyo kutoka 2007 hadi 2011.
Naftali alikaririwa akisema kwamba, matamshi hayo ya kibaguzi
yaliondolewa katika mawasiliano wakati kanda hiyo ilipotolewa 2000 na makavazi
ya kitaifa kwa sababu za faragha-wakati rais Reagan bado alikuwa hai. Miongoni
mwa nukuu ya mahiri, “Serikali si suluhisho la matatizo yetu; serikali ndiyo
tatizo.” Reagan aliisema katika hotuba
yake ya kuapishwa kuwa rais wa 40 wa Marekani.
Alizaliwa Februari 6, 1911 mjini Tampico, Illinois nchini
Marekani na kufariki dunia mjini Bel-Air Los Angeles jimboni California. Kabla hajawa
gavana wa 33 wa jimbo la California alilohudumu kutoka mwaka 1967 hadi 1975,
Reagan alikuwa mwigizaji wa Hollywood.
Mwandishi wa gazeti la Washington Post wakati huo William
Gildea aliandika mengi kumhusu Reagan katika medani ya michezo katika gazeti
hilo. Aliandika michezo ilikuwa ndani ya damu ya Ronald Reagan. Reagan aliwahi
kukaririwa akisema tangu enzi za ujana wake alikuwa akipenda kuigiza, siasa na
michezo.
Reagan alikulia katika mji mdogo wa Illinois. Alipokuwa
akisoma alikuwa akicheza soka katika Shule ya Dixon ambako alihitimu mwaka
1928. Pia Reagan alikuwa muogoleaji, akipendelea zaidi majira ya joto miaka ile
ya 1927 hadi 1932. Ilirekodiwa kuwa Reagan katika medani ya kuogolea aliwaopoa
watu 77 waliotaka kuzama kwenye maji. Alifanya hayo katika chuo cha Eureka hapo
hapo Illinois karibu na Peoria wakati huo akicheza soka.
Mbali ya soka alikuwa mwendeshaji wa farasi mzuri na
alipokuwa Dixon alikuwa akiangalia sana filamu za Tom Mix ambaye alikuwa
akimpenda. Hakuishia hapo aliendelea hata miaka mingi iliyofuata.
Reagan hakuweza kucheza Baseball licha ya kusoma na mkali wa
mchezo huo wa zama zote Babe Ruth kutokana na kuwa na uoni wa karibu ambao
aligunduliwa katika miaka ya ujana wake hali iliyokuwa ikimnyima fursa ya kuona
vizuri mipira kwenye dimba hadi awe
karibu sana na tukio.
Mwaka 1932 alihitimu katika chuo cha Eureka ambako Reagan alikuwa akijua kuwa hana mpango wa kuwa mwanamichezo lakini alijiwekea malengo
kuwa ataweza kuwa mtangazaji wa michezo.
Hali hiyo alitiwa moyo sana na mama yake tangu akiwa shule ya
sekondari na chuoni. Ndoto zake zilitimia pale alipokuwa miongoni mwa
watangazaji wa redio akipata kazi ya kutangaza michezo pale WOC, Davenport
jimboni Iowa pale aliposimama mbele ya kipaza sauti na kutangaza mchezo husika.
0 Comments:
Post a Comment