Juni 17, 1972 ulikuwa mwanzo wa kashfa ya Watergate ambao ulianza kwa watu watano kutiwa nguvuni kwa kujipenyeza kwenye Kamati Kuu chama cha Democratic na kuvujisha siri za vikao vya kamati hiyo.
Wakati wanakamatwa walikutwa na zana za kuvunjia, kamera na miakanda ya video. Baada ya uchunguzi ikabainika kuwa watuhumiwa walikuwa timu ya uchaguzi ya Rais Richard Nixon wa Republican ambaye baadaye alijiuzulu kwa kashfa hiyo.
Siku ya tukio ilianza hivi ambapo nyakati za usiku wa kuamkia Jumamosi ya Juni 17, 1972 mlinzi wa Watergate Complex aliyefahamika kwa jina la Frank Wills aligundua kuwa kuna vinasa sauti vilikuwa vimefungwa katika vitasa vya milango kuanzia kwenye eneo la chini la kupaki magari. Lakini mikanda hiyo ilifungwa kwenye vitasa hivyo ilikuwa ikiruhusu milango kufunguka na kujifunga.
Baada ya kuzungukia eneo lake aliporudi alikuta mikanda ile imeondolewa hivyo ikabidi awaite polisi. Wito wa simu yake uliwafikia Maafisa wa Jeshi la Polisi watatu (Sajenti Paul W. Leeper, Afisa John B. Barrett, na Afisa Carl M. Shoffler)ambao waliokuwa zamu siku hiyo, waliamua kwenda. Wakiwa wamevalia kama wauzaji wa dawa za kulevya kwani siku hiyo walikuwa katika kikosi maalum cha kufuatilia wanaojihusisha na biashara hiyo.
Alfred Baldwin ambaye alikuwa akisimamia kitengo cha kamera katika jengo hilo alizuiwa asione ujio wa gari la polisi upande wa mbele wa jengo hilo. Pia akiwa hapo hakufanikiwa kuwaona maafisa waliovalia nguo za kiraia walioingia na kuanza uchunguzi wao katika ghorofa ya sita.
Hata hivyo Baldwin aligundua kuwa kuna jambo ambalo sio la kawaida linaendelea katika ghorofa ya sita hata hivyo alikuwa amechelewa kwani Polisi walishawahi na kuwatia nguvuni watu watano ambao Virgilio Gonzalez, Bernard Barker, James McCord, Eugenio MartĂnez, na Frank Sturgis. Watuhumiwa hao walikamatwa na kupandishwa kizimbani kwa majaribio ya kutaka kuvunja na kufanya udukuzi.
SABABU ZA KASHFA YA WATERGATE
Ilikuwa hivi! Watergate ni jina la moja ya hoteli ya kifahari hapo jijini Washington DC katika ufukwe wa bahari ya Atlantiki.
Kashfa hii ilitokana na uchaguzi wa urais wa Marekani mwaka 1972, uliomweka madarakani Rais wa 37 wa Marekani Richard Nixon kwa tiketi ya chama cha Republican.
Chama cha Republican kilikuwa na dalili zote kushindwa kutokana na kukosa imani kwa wananchi wa Marekani hususani baada ya taifa hilo kushindwa katika Vita ya Vietnam. Kutokana na sababu hiyo ushawishi na mvuto wa Republican kabisa machoni mwa Wamarekani kwani Vita ya Vietnam kule Hanoi na Saigon kuliionyesha namna majeshi ya Marekani yalivyokuwa yakitimika yenyewe hali ambayo ilikuwa ni ya aibu kwa Marekani yote.
Republican haikuwa tayari kabisa kushindwa uchaguzi huo kwa hiyo walifanya kila mbinu washinde, hizo mbinu ndizo zilizaa kashfa ya Watergate.
Katika hoteli hiyo ya kifahari Democratic ilikuwa ikifanya mikutano ya kimbinu kwa ajili ya kukimaliza chama cha Republican, walikuwa wakijadili mbinu gani za ushindi wanatakiwa wazitumie ili kushinda uchaguzi. Mojawapo ya mbinu hizo ni kujua Democratic walikuwa wanajadili mbinu gani za ushindi katika ukumbi wa mkutano wa Hotel ya Watergate?
Walichofanya walipeleka watu wao wakatege kanda za kunasa mazungumzo ya wapinzani wao ndani ya mikutano ili wazijue mbinu zao pia kunasa mawasiliano yao ya simu. Kwa hili walifanikiwa ila Democratic walianza kushangaa kwa nini kila wanachopanga Republican wanajua na wanatekeleza kila walichoazimia?
Kwa bahati mbaya vyombo walivyotega viliacha kufanya kazi na inakisiwa kuwa chama cha Democratic kiligundua mtego huo kikategua na wenyewe Democratic wakatega mtego. Hata hivyo Republican wakarudi tena Watergate na kutengeneza hiyo hitilafu ili mawasiliano yawafikie tena Repulican, ni kama unaenda kuiba mwenyewe anakuona, Democratic wakapiga simu polisi wale jamaa walikamatwa wakifanya hiyo kazi na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Hatimaye Republican walishinda ila Democratic walifungua kesi ya udukuzi kwa kutumia mpelelezi wao binafsi waliwabana vilivyo Republican kwa kutumia kanda walizozinasa na zingine zilikuwa tayari ziko kwenye chama tawala ambapo mahakama iliamuru kiongozi wao Richard Nixon azitoe kama ushahidi, alikataa kwani kwa kufanya hivyo ni kama kupeleka ushahidi Polisi.
Kwa sheria za Marekani ilibidi Rais Nixon ajiuzulu ili ashitakiwe mahakamani kwa kashfa hiyo. Rais Nixon alifanya hivyo na makamu wake Gerard Ford aliendeleza urais wake na akamsamehe Rais wake asishitakiwe mahakamani.
Wakati Rais Nixon akijiuzulu kwa huzuni kuu alisema, “Kwa kuchukua hatua hii nitakuwa nimeharakisha hatua ya mwanzo ya uponyaji wanayohitaji Wamarekani.”
Baada ya Rais Nixon kujiuzulu watu wakajua Kashfa ya Watergate imeisha lakini maswali yalikuwa mengi yasiyo na majibu kutokana na namna suala hilo lilivyoanza hadi kumalizika.
DEEP THROAT AJIWEKA HADHARANI
Hata hivyo Mei 31, 2005 Afisa wa zamani wa shirika la ujasusi la Marekani (FBI) William Mark Felt Sr. alikiri kwamba alikuwa na jukumu kubwa katika kusaidia kumporomosha rais wa zamani wa Marekani, Richard Nixon, katika kashfa ya Watergate.
Wakati akianika ukweli huo Mark Felt alikuwa na umri wa miaka 91, na wakati wa kasfa hiyo alikuwa makamu kiongozi wa shirika hilo katika miaka ya mwanzo ya 1970.
Afisa wa FBI aliyetajwa kwa jina la ´Deep Throat´ wakati huo aliwasaidia waandishi wa gazeti la Washington Post, Bob Woodward na Carl Bernstein, kwenye uchunguzi wao katika kashfa ya Watergate, ambayo hatimaye ilipelekea kujiuzulu kwa rais Nixon mwaka wa 1974.
Mark Felt alifariki dunia miaka mitatu baadaye Desemba 18, 2008 akiwa na umri wa miaka 95. Woodward na Bernstein walikiri kwamba Mark Felt ndiye aliyekuwa Deep Throat, hivyo kutoa jibu kwa suala lililosumbua kwa miongo kadhaa.
Nixon alifariki dunia mnamo April 22, 1994 huko New York City akiwa na umri wa miaka 81. Gerard Ford alifariki dunia Desemba 26, 2006 huko Rancho Mirage, California akiwa na umri wa miaka 93.
0 Comments:
Post a Comment