Juni 22, 1593 kuliibuka vita
baina ya majeshi ya Ottoman chini ya Kamanda Telli Hassan Pasha ambaye alikuwa
maarufu katika ukanda wa Eyalet huko Bosnia na majeshi ya muungano ya Kikristo
kutoka ardhi ya Habsburg (Croatia na Austria).
Vita hiyo ilipiganwa katika eneo la
Sisak katikati ya Croatia ambapo kuna maungio ya mito ya Sava na Kupa. Mapema
mwaka 1591 na 1592 majeshi ya Ottoman yalishindwa mara mbili jaribio la kutaka
kuichukua Sisak lakini walifanikiwa kuichukua Bihac mnamo mwaka 1592.
Ngome ya Sisak ilianza kuzungukwa
tena mnamo Juni 15, 1593. Makamanda wa Kijeshi wa Sisak Blaž Đurak na Matija
Fintić wote walikuwa ni kutoka katika wilaya ya Zagreb. Jeshi likiwa chini ya
Kamanda Mkuu Jenerali Ruprecht von Eggenberg kutoka Austria lilikusanyika
haraka ili kuharibu mipango ya Kamanda Pasha.
Majeshi ya Croatia yalikuwa
yakiongozwa na Thomas Erdody na yale ya Carniola na Carinthia yaliongozwa na
Andrea von Auersperg ambaye alikuwa akifahamika kama Carniolan Achilles.
Majeshi hayo ya Sisak yaliwafanyia ‘surprise’
yaani shambulio la ghafla wakiwa bado wapo pembezoni mwa ngome hiyo na
kuyazabua majeshi ya Ottoman.
0 Comments:
Post a Comment