Juni 29, 1969 alifariki dunia mwanasiasa wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Moise Tshombe.
Mwanasiasa huyo alikuwa Rais wa
kwanza wa jimbo lililotaka kujitenga Lenye utajiri wa madini ya shaba la
Katanga huko DRC. Pia alikuja kuwa Waziri Mkuu wa DRC.
Alifariki dunia jijini Algiers, Algeria akiwa na umri
wa miaka 49. Mnamo mwaka 1967, Tshombe
alihuhukumiwa kifo bila yeye mwenyewe kuwepo (in absentia).
Juni 30, 1967 akiwa nadani ya ndege ya Hawker Siddeley
ambayo ilitekwa na Francis Bodenan ambaye alikuwa wakala wa ujasusi wa SDECE ya
Ufaransa. Kwa mujibu wa taarifa za serikali ya DRC wakati huo zilisema kuwa, Tshombe
alikuwa akienda Afrika.
Tshombe alipelekwa Algeria ambako alitupwa jela na
kuwekwa chini ya ulinzi mkali. Marubani wa ndege Britons Trevor Coppleston na
David Taylor waliachiliwa na walirudi zao nchini Uingereza.
Serikali ya DRC ilikuwa ikitaka arudishwe nchini mwake
lakini ilishindikana kutokana na waungaji mkono wake wa Kimagharibi walikataa
kuachiliwa kwake. Algeria nao walikataa maombi yote mawili ya DRC na waungaji
mkono wa Kimagharibi.
Kamati maalumu ya Tshombe iliyokuwa nchini Marekani ikiongozwa
na Marvin Liebman na William F. Buckley walianza harakati za kushinikiza
Tshombe kuachiliwa na kupelekwa nchini Hispania.
Rafiki mkubwa na mtoaji wa misaada wa Tshombe
aliyefahamika kwa jina la Michel Struelens alisafiri katika miji tofauti barani
Ulaya ili kupata uungwaji mkono wa sehemu ya kumweka Tshombe lakini hakupata
msaada.
Tshombe alifariki dunia kwa kile kilichoelezwa mshtuko
wa moyo huko Algiers. Tshombe alizikwa katika makaburi ya Etterbeek karibu na
Brussels nchini Ubelgiji.
Tshombe kama alivyokuwa Patrice Lumumba amekuwa
akichukuliwa kuwa alama muhimu katika mapambano dhidi ya uzalendo wa Mwafrika.
Mwanadiplomasia wa DRC Thomas Kanza mnamo mwaka 1972
alikaririwa akimwelezea Tshombe alikaribia kuwa mkombozi wa DRC. “Moise Tshombe
alikaribia kuwa mwokozi wa Congo wakati akirudi kutoka uhamishoni. Lakini
historia iliamua vinginevyo na watu wa Congo walijikuta wakiwa chini ya uongozi
wa Mobutu.”
Jina lake halisi ni Moise-Kapenda Tshombe. Alizaliwa
Novemba 10, 1919 katika mji mdogo wa Musumba katika ardhi ya DRC wakati huo
ikiitwa Belgian Congo. Aliamua kujitenga na kuwa kiongozi wa jimbo la Katanga
mnamo mwaka 1960.
Alipata nguvu ya kujitenga kutokana na nguvu za
kijeshi kutoka kwa washirika wake. Kwa miaka mitatu alifanikiwa kuisimamia
ardhi huru ya Katanga akiungwa mkono na Umoja wa Mataifa. Tshombe alikuwa
mwanasiasa mwenye akili katika siasa za DRC enzi za uhai wake.
Mnamo mwaka 1963 majeshi ya UN yaliivamia Katanga na
kumwondoa Tshombe ambaye alikimbia uhamishoni Northern Rhodesia (Zambia) na
baadaye alikwenda Hispania.
Mnamo Julai 1964 alirudi nchini DRC ambako alihudumu
kama Waziri Mkuu wa serikali mpya ya Muungano. Baraza lake liliapishwa Julai
10.
Tshombe alikuwa akiungwa mkono na wanasiasa wa majimbo
ya DRC, machifu na wenye fedha kutoka nje.
Aliposhika nafasi hiyo jambo la kwanza alilolifanya ni
kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa 600 akiwamo Antoine Gizenga na aliamuru wanajeshi
wa Katanga waliokimbilia Angola kurudi DRC na kuungana na jeshi la taifa hilo.
Katika hotuba yake ya Mwaka Mpya mnamo mwaka 1965,
Tshombe alikataa kuungana na Waasi wa Simba ambao walikuwa wafuasi wa Lumumba.
Aliondolewa katika Uwaziri Mkuu wa DRC mnamo Oktoba
1965 na Rais Joseph Kasavubu. Mwezi Novemba ikiwa ni mwezi mmoja baada ya
kuondolewa katika nafasi hiyo Jenerali Mobutu Sese Seko alifanya jaribio
lililofanikiwa na kumwondoa madarakani Kasavubu.
0 Comments:
Post a Comment