Wapigania haki za Raia waliuawa katika Kaunti ya
Neshoba huko Mississippi ambapo Andrew Goodman, James Chaney na Michael
Schwerner. Goodman aliuawa akiwa na umri wa miaka 20, Chaney aliuawa akiwa na
umri wa miaka 21, Schwerner aliuawa akiwa na umri wa miaka 24.
Wanaharakati
hawa waliuawa wakati wakiwa kwenye vuguvugu la Freedom Summer ambalo
lilizinduliwa rasmi Juni 1964.
Kampeni hiyo ya kujitolea ilikuwa ikitaka haki
kwa Wamarekani weusi kuwa na haki ya kupiga kura katika jimbo la Mississippi.
Wamarekani weusi hawakuruhusiwa kupiga kura hapo kabla.
Wanaharakati hao vijana
waliendesha vuguvugu hilo mnamo mwaka 1962 ilikuwa ni asilimia 5.3 pekee ya
Wamarekani weusi walikuwa na haki ya kupiga kura huko Mississippi.
Wanaharakati
hawa waliuawa na Ku Klux Klan ambalo lilikuwa ni kundi la Wamarekani weupe
ambalo liliundwa kwa ajili ya kukomesha uwepo na shughuli zote za Wamarekani
weusi.
Vuguvugu hilo lilisababisha kuundwa kwa Baraza la Vyama vya Shirikisho
(COFO), kuundwa kwa shule za kiharakati kudai haki hizo, kuundwa kwa chama cha
MFDP cha Mississippi, na ilikuwa alama muhimu kwa wakati wa kupitishwa kwa sheria
ya kuhusu haki ya kupiga kura (Voting
Rights Act of 1965).
Mwanzilishi wa vuguvugu hilo lililosababisha wanaharakati
vijana kuuawa ni Bob Moses. Mwanzilishi huyo alikuwa katibu mkuu wa chama cha
SNCC na mkurugenzi msaidizi wa COFO wakati vuguvugu hilo.
Bob Moses alikuwa na
miaka 28 alipoendesha vuguvugu hilo kwa sasa (2020) Bob Moses ana umri wa miaka
85, akiendelea na utoaji wa elimu na kuendesha harakati mbalimbali za usawa
katika jamii nchini humo.
Kiongozi wa kundi la Ku Klux Klan miaka hiyo ya 1960 aliyeamuru mauaji ya wanaharakati Edgar Ray Killen miongo minne (miaka 41), baadaye alikamatwa na kutupwa jela ambako alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 92 mnamo mwaka 2018.
Killen alifariki dunia majira ya saa 3 usiku
wa Januari 11, 2018 wakati akitumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa mauaji hayo James
Chaney, Michael Schwerner na Andrew Goodman.
0 Comments:
Post a Comment