Juni 10, 323 KK alifariki dunia mfalme wa Macedonia Alexander the Great. Alexander alikufa katika jumba la kifalme la Nebuchadenezzar II, mjini Babeli, akiwa na umri wa miaka 33. Kulikuwa na simulizi mbili juu ya kifo hicho, hata maelezo ya kifo yanatofautiana kidogo.
Maelezo ya Plutarch ni kuwa takriban siku 14 kabla ya
kifo chake, Alexander alimkaribisha askari wa jeshi la majini Nearchus, alikaa
naye usiku mzima na siku ya pili yake wakiwa wanakunywa pamoja na Medius wa
Larissa (huyu alitoka familia katika familia mashuhuri na alikuwa rafiki wa
Alexander).
Baada ya hapo Alexander alipata homa iliyoendelea
mpaka alishindwa kuongea. Askari wa chini, wakiwa na shauku juu ya afya yake,
walipewa ruhusa ya kupita mbele yake huku akiwapungia mkono taratibu.
Maelezo ya pili ni kutoka kwa Diodours ambayo yanasema
kuwa Alexander alianza kusikia maumivu baada ya kunywa bakuli kubwa la mvinyo
bila kuuchanganya, kwa heshima ya Heracles, hii ilifuatia siku 11 za ugonjwa na
kupoteza nguvu, hakupata homa ila alikufa baada ya maumivu makali.
Arrian pia anaelezea hadithi hii lakini Plutarch
alikataa kabisa maelezo haya. Kupitia madai ya watu wa hadhi ya juu wa
Macedonia ni kuwa kifo cha Alexander kilisababishwa na mauaji. Kuanzia
Diodorus, Plutarch, Arrian na Justin wote wanaelezea uwezekano wa kuwa
Alexander aliwekewa sumu.
Justin anaeleza kuwa Alexander alikuwa mhanga wa
jaribio la sumu, Plutarch anapinga hili na kusema ni uongo uliotengenezwa,
wakati Diodorus na Arrian wote wanasema maelezo haya yamewekwa kama hitimisho
la kifo.
Antipater alipinga kifo cha Alexander kuwekewa sumu na
mtoto wake Iollas ambae alikuwa mhudumu wa mvinyo wa Alexander.
Mabishano makali yaliendelea kuwa kama ilikuwa sumu
isingeweza kuchukua siku 12 kumaliza maisha ya Alexander; wengine wanadai
ilikuwa sumu iliyoua taratibu.
Hata hivyo mwaka 2003 Shirika la Utangazaji la
Uingereza (BBC) walionyesha documentary iliyokuwa na uchunguzi wa kifo cha
Alexander, Leo Schep kutoka New Zealand National Poisons Center alielezea mmea
mweupe uitwao hellebore (Veratrum album), ambao ulijulikana kwa nyakati zile,
inawezekana ulitumika kama kumuulia Alexander.
Mwaka 2014 jarida la Clinical Toxicology, Schep
aliandika uwezekano wa mvinyo aliokunywa Alexander kuwa uliwekewa sumu ya
Veratrum album, kwa kuwa sumu hiyo inatoa dalili zote za kifo kinachoripotiwa
juu ya Alexander katika kitabu cha "Alexander Romance".
Sumu ya Veratrum inatoa matokeo taratibu na
inawezekana kama Alexander aliwekewa sumu hiyo, inawezekana ikawa sababu kubwa
ya kifo. Sababu nyingine kubwa ya kifo inayoelezewa mwaka 2010 ni kuwa,
mazingira ya kifo chake yalitokana na maji ya mto Styx (kwa sasa unafahamika mto
Mavroneri nchini Ugiriki), ambao inasemekana ulikuwa na sumu ya calicheamicin
ambayo ni compound inayotoka kwenye bacteria.
Sababu nyingi zilizoweza kusababisha kifo cha
Alexander zilielezewa, ikiwemo uwezekano wa kuugua malaria au typhoid.
Mwaka 1998 chapisho la New England Journal of Medicine
lilielezea kifo hicho kuwa kilisababishwa na homa ya typhoid na ilikuwa mbaya
zaidi kwa kuwa ilimletea kuwa na vidonda kwenye utumbo na kusababisha neva za
fahamu kupoteza nguvu.
Uchunguzi mwingine unaelezea pyogenic infection
spondylities au meningitis au uti wa mgongo. Wengine wanasema alipata maumivu
makali kutokana na kushambuliwa na virusi vya West Nile virus. Maelezo mengine
ni kuwa, afya ya Alexander inawezekana ilianza kudhoofika kwa muda mrefu baada
ya miaka mingi ya kunywa mvinyo na pombe kali na pia vidonda na majeraha.
Pia majonzi aliyoyapata baada ya kifo cha Hephaestion ambaye
alikuwa Jenerali wa Jeshi la Alexander na rafiki yake mkubwa inawezekana
yamechangia kifo chake, kwa kumletea sonona.
0 Comments:
Post a Comment