Umoja wa Ulaya (EU) umesema upo tayari kuwa mwangalizi wa
uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020 nchini Tanzania, endapo
watapata ridhaa kutoka katika mamlaka husika.
Balozi wa Umoja wa Ulaya kwa nchi za Afrika Mashariki
Manfredo Fanti alisema hadi sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika baina
ya taifa hilo la Afrika mashariki pamoja na jumuiya hizo ya kimataifa kuhusiana
na suala la uchaguzi, ijapokuwa upo tayari kufanya uangalizi wa uchaguzi huo
ambao utawaweka mamlakani, madiwani, wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Aidha Balozi Fanti alisema taifa lina jukumu la
kuhakikisha kunakuwa na uchaguzi huru, haki na amani katika kipindi chote cha
uchaguzi, huku akisisitiza kuwa umoja huo hauna mamlaka ya kuangalia uchaguzi
bila mamalaka husika kutoa idhini.
Itakumbukwa kuwa sehemu ya kanuni za uchaguzi
zinaeleza kuwa, Tume inaweza kutuma mwaliko kwa waangalizi wa kimataifa, jambo
ambalo lilitoa wasiwasi kwa vyama vya siasa hasa upinzani kwamba huenda NEC
isitoe fursa hiyo kwa jumuia za kimataifa kufuatilia kwa ukaribu zoezi hilo la
kidemocrasia kama ilivyofanyika kwa chaguzi zilizopita.
CHANZO: DW
0 Comments:
Post a Comment