Julai 6, 2019 alifariki mwanaanga wa kwanza mwafrika kudhamiria
kwenda katika anga za juu raia wa Afrika Kusini Mandla Maseko.
Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 30 jijini
Pretoria. Alifariki dunia kwa ajali ya pikipiki. Alizaliwa huko Soshanguve
nchini Afrika Kusini kaskazini kwa jiji la Pretoria mnamo Agosti 27, 1988.
Alikuwa mtengenezaji wa vifaa vya moto na mfanya usafi katika shule.
Pia alikuwa mwanafunzi wa Jeshi la Anga la Afrika
Kusini. Akiwa katika jeshi la Anga alikuwa rubani wa ndege ambaye alikuwa na
cheti cha kuongoza ndege peke yake (PPL). Alikuwa DJ na pia mwendesha mzuri wa
pikipiki.
Mnamo mwaka 2013 alikuwa miongoni mwa washindi 23
walioingia katika mashindano katika Akademi ya Axe Apollo Space. Mamilioni ya
washiriki walishiriki mashindano hayo ambaye Maseko alipata nafasi ya kwenda
nchini Marekani katika Akademi ya Masuala ya Anga ya Marekani ili awe Mwafrika wa
kwanza kwenda katika anga za juu.
Alikuwa akifahamika kwa jina la Afronaut au Sapceboy.
Alikwenda Kennedy Space Center mjini Florida kwa juma moja kwa ajili ya
majaribio kama vile skydiving na safari inayofahamika kama Reduced-Gravity
Aircraft pia mpango wa saa moja wa suborbital flight katika chombo aina ya XCOR
Lynx Mark II ambayo ilipangwa kufanyika mwaka 2015 licha ya kwamba mpango huo
haukufanikiwa kutokana na waratibu wa safari hiyo ya mwezini XCOR Aerospace
kufilisika mnamo mwaka 2017.
Maseko alirejea kikosini na kufanya kazi kama rubani
wa kujitegemea. Kila alipokuwa akipata muda alikuwa Dj na pia aliendesha baiskeli.
0 Comments:
Post a Comment