Friday, July 31, 2020

Eid ul-Adha: Bakwata Kilimanjaro yatoa wito kuelekea uchaguzi mkuu 2020

Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Kilimanjaro limewataka viongozi wa dini mkoani humo kutojihusisha na masuala ya siasa kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu na badala yake wajikite kuhubiri kuhusu amani na upendo miongoni mwa watanzania.

Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Kilimanjaro Sheikh Shaban Mlewa,

Sheikh Mlewa alisema Taifa linakwenda kuingia kwenye uchaguzi hivyo ni vyema wakamkumbuka muumba kwa ajili ya kuwapatia kiongozi mwema atakaye kwenda kuwaletea maendeleo Watanzania wote.

“Viongozi wa dini wajitenge na mambo ya kuingizwa katika mambo ya siasa hususan katika kuelekea uchaguzi wa Oktoba ikiwemo masuala ya rushwa au kupendelea upande mtu fulani,”alisema Sheikh Mlewa.

Aidha aliwataka wananchi kukataa kurubuniwa kwa kupewa rushwa ya aina yoyote ili waweze kumchagua kiongozi kwani mtu huyo hataweza kuleta maendeleo na badala yake atakapopata fursa hiyo ataanza kwanza kurudisha gharama zake alizozitumia wakati wa kuomba kura.

Kauli mbiu katika Eid el Adha ni

Hata Sheikh Mlewa alisema

“Eid el Adha ndiyo sikuu ya kuu zaidi ya kidini miongoni mwa waislamu kote duniani ambayo huambatana na mapumziko kwenye mataifa mengine yenye waislamu.

Eid al-Adha ndiyo sikukuu kuu zaidi ya kidini miongoni mwa Waislamu kote duniani na pia huwa ni siku ya mapumziko mataifa mengi yenye Waislamu. Imekuwa na majina mbalimbali katika mataifa ya Kiislamu,


0 Comments:

Post a Comment