Janga la Njaa la Ireland (Irish Potato) lilianza hivi;
mnamo mwaka 1845 kuliibuka kwa fangasi aina ya Phytophthora infestand au P.
infestans ambao walisambaa katika ardhi ya Ireland. Fangasi hao walivamia viazi
mviringo mwaka huo na robo tatu ya zao hilo kwa miaka saba iliyofuata.
Wakulima wa Ireland ambao walikuwa wakitawaliwa na
Uingereza viazi mviringo vilikuwa ndio chakula chao kikuu. Kuvamiwa kwa
mashamba hayo na viazi hivyo kuharibiwa lilikuwa ni janga ambalo
halitasahaulika katika historia ya watu wa Ireland.
Kabla ya kuisha kwake mnamo mwaka 1852 vifo
vilivyotokana na kupotea kwa viazi mviringo
viliathiri Ireland kwani wengi walipoteza maisha kutokana na ukosefu wa
chakula na mamilioni ya watu walijikuta wakiondoka katika ardhi hiyo na kwenda
kuishi kama wakimbizi ili kuponya uhai wao.
Kutokana na kupitishwa kwa sheria ya Muungano mnamo
mwaka 1801, Ireland ilikuwa ikishikiliwa kama koloni la Uingereza hadi wakati
wa Vita vya Uhuru mapema katika karne ya 20. Mataifa hayo mawili yaliungana
tena na kutengeneza kile kinachofahamika kama United Kingdom of GB na Ireland.
Kupitia sheria hiyo serikali ya Uingereza iliteua
wasimamizi ambao walikuwa ni Lord Liutenat na Chief Secretary wa Ireland huku
wakazi hao wakipewa nafasi ya kuchagua wawakilishi wao katika bunge la London.
Ireland ailipeleka wawakilishi 105 katika bunge dogo (House Commons) na 28 ambao
wengi wao wakiwa makabaila walipelekewa katika Bunge kubwa (House of Lords).
Miaka 100 kabla ya janga la njaa, zao la viazi
mviringo Ireland lilikuwa likistawi na kuonekana ni chakula wenye uwezo mdogo
(maskini) na maskini hao walikuwa wakisaidika zaidi wakati wa majira ya baridi.
Wakati fangasi hao wakivamia zao hilo viongozi wa Ireland jijini Dublin
walipeleka malalamiko yao kwa Malkia Victoria na Bungeni kuhusu sheria.
Hali ambayo ilisababisha kuundwa kwa sheria za mazao
ya nafaka ‘Corn Laws’ ambapo tozo katika nafaka zilitakiwa kushuka ili watu waweze
kununua walau hata mkate kwa ajili ya kujikimu. Hata hivyo mabadiliko hayo
hayakusaidia kwani wakulima wengi walikuwa hawana uwezo wa kuzalisha chakula
cha kutosha kwa ajili ya matumizi yao.
Hali hiyo ilisababisha vitu kupanda bei na maelfu walifariki
dunia kutokana na ukosefu wa chakula, pia wengine walijikuta wakiangukia kwenye
magonjwa yaliyotokana na utapiamlo. Wanahistoria wanasema wakati wa janga hilo
Ireland ilikuwa ilikiendelea kuingiza chakula kwa wingi nchini humo kutoka GB.
Mifugo na mazao yatokanayo na mifugo yaliongezeka
katika kipindi hicho cha Irish Potato. Mnamo mwaka 1847 rekodi zinaonyesha
bidhaa kama njegere, maharage, sungura, samaki, samaki na asali vilikuwa vikiendelea
kuingizwa huko Ireland licha ya njaa kuikumbuka ardhi hiyo.
Viazi mviringo vilianza kurudi tena baada ya mwaka
1852 baada ya janga hilo, huku ikikadiriwa kuwa wake kwa waume na watoto
wapatao milioni moja wanadaiwa kupoteza maisha kutokana na njaa hiyo. Pia watu
wapatao milioni moja walihama Ireland kwa ajili ya kukimbia umaskini na ukosefu
wa chakula ambapo wengi wao walikimbilia Amerika Kaskazini na Uingereza.
Wakati Waziri Mkuu Tony Blair alipokuwa madarakani
mnamo mwaka 1997 aliomba radhi kwa Ireland kutokana na serikali ya Uingereza
kushindwa kulibeba suala hilo wakati huo. Katika maeneo kama Boston, New York
City, Philadelphia na Phoenix nchini Marekani pia Montreal na Toronto nchini
Canada, wamekuwa wakifanya kumbukizi ya janga hilo sambamba na miji kadhaa huko Ireland,
Australia na Uingereza.
Aidha kumbukizi hii iliwahi kufanywa na klabu ya soka
ya Celtic ya jijini Glasgow mano Septemba 30. 2017 ikiwa sehemu ya kukumbuka
madhara yaliyojitokeza kutokana na uvamizi wa fangasi hao katika viazi
mviringo.
0 Comments:
Post a Comment