Mbunge aliyemaliza muda wake wa Moshi Mjini Mkoani
Kilimanjaro Jaffary Michael ameweka kinagaubaga masikitiko yake kuhusu miaka
mitano ya kuliongoza jimbo hilo hususani dhamira ya kuufanya mji wa Moshi kuwa
jiji miongoni mwa mengine nchini.
Akizungumza katika mahojiano maalum Mbunge huyo wa zamani aliweka bayana kuwa hataweza kuwania tena nafasi ya ubunge kwa namna yoyote ile licha ya kuwa na nafasi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
“Nilishasema tangu mwaka 2016 mimi sitagombea ubunge, kwa jimbo la Moshi mjini, ninazo sababu kuu mbili. Ilionekana kama vile mimi ninafaidika sana na dani ya chama change, kwa sababu huu utumishi ni wito na sitaki uwe ni vita, nimeamua kwa kipindi change cha miaka mitano nipumzike ili nawengine waweze kuja kuendea nilipoishia. Mambo yangu ya kifamilia nilitaka niyaweke sawa , hivyo uwamuzi wangu ni kutokugombea tena jimbo la Moshi mjini kwa kipindi cha mwaka 2020 ndio msimamo wangu,” alisema Jaffary.
Aidha Jaffary aliongeza kuwa vikwazo ndani ya Chadema ndivyo vimemfanya kuachana na mbio hizo kwa awamu nyingine ili kuwa na Amani moyoni mwaka.
“Mimi kitu ambacho kilinikwaza sana katika Ubunge wangu, ni tabia za viongozi wangu ndani ya chama, mimi sina ugomvi na wananchi wangu wa Moshi, sinatatizo na ubunge, . watu ukichaguliwa wanaamini kwamba wewe ndie chanzo chao cha kipato, unakuwa mzigo wa kuwa kiongozi,” alisema mbunge huyo.
Jaffary alisisitiza kuwa mapambano ya ndani ya Chadema ya wenyewe kwa wenyewe yalizidi kuharibu utendaji wake kipindi chote cha ubunge wake.
“Wewe uko ndani ya familia moja halafu mnalazimika kupambana ninyi wenyewe halafu kuna jirani yenu wan je ambaye naye anashindana na nyinyi sasa hiyo vita hamtakaa mshinde. Kuna baadhi ya viongozi wangu ndani ya chama hawakuridhishwa na mimi kuwepo kwenye hiyo nafasi, kwa nini na mimi nilazimishe kuendelea kuwepo hapo,” alisisitiza Jaffary.
Hata hivyo utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt John Pombe Magufuli hususani kudhibiti fedha za umma na ujenzi wa reli ya mwendokasi (SGR) imekuwa chachu kubwa kwa jamii ya Watanzania kwa ujumla.
Jaffary alisema anaondoka katika nafasi hiyo hatarajii kwenda chotechote isipokuwa kinachomsikitisha ni Moshi Mjini kuwa jiji kama yalivyo Dar es Salaam, Dodoma, Tanga na Mwanza.
“Moja ya changamoto kubwa ambayo kwangu mimi sitaweza kuisahau ni kushindwa kutimiza ahadi yangu ya Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kuwa Jiji, nimehuzunika sana kwa sababu tulitumia fedha za wananchi kuelimisha watu ili wakubali kutoa maeneo yao na katika mchakato wote wa Moshi kuwa Jiji. Ni bahati mbaya wakati tukiwa katika hatua za mwisho ile ndoto ya Moshi kuwa Jiji ilizimwa ghafla,” alisema Jaffary.
Mbunge huyo aliyemaliza muda wake aliongeza kusema, Hii ilikuwa moja ya ahadi yangu kubwa kwa wananchi Jiji lingesaidia kuinua utalii wetu wa Moshi, ubora wa elimu, uchumi wetu,” alisema
0 Comments:
Post a Comment