Mpira wa miguu ni mchezo ambao umetia fora duniani
kote. Katika baadhi ya nchi hususani za Amerika Kusini, kandanda ni ndio kila
kitu. Ushindi huleta furaha na starehe, hata wakati wa shida, kushindhwa huleta
simanzi na vurugu wakati mwingine hata ikiwa ni wakati wa nnema.
Zipo hadithi nyingi za kufurahisha na kusikitisha
ambazo chanzo chake ni mpira wa mviringo unaochezwa kwa miguu maarufu kabumbu,
soka. Wapo baadhi ya watu wamegombana, mke na mume kutengana au kutalikiana
kwasababu ya mapenzi makubwa katika soka.
Lakini katika yote hayo, kilichotia fora ni wakati
nchi za Amerika zilipopigana vita na mamia ya watu kupoteza maisha kutokana na
uhasama wa mpira wa miguu kati ya timu mbili za mataifa hayo. Historia ya soka
ni ndefu mno na yenye kutatanisha katika baadhi ya mambo.
Hata hivyo wanahistoria wengi wa michezo wanakubali
kwamba ushahidi wa kwanza wa mchezo huu ulipatikana nchini China. Inaelezwa
huko ulikuwa ukijulikana kama Tsuhalic-Chu katika nyaraka za historia za miaka
elfu iliyopita. Neno Tsuhalic maana yake kupiga. Na Halic-Chu ina maana ya
mpira.
Siku hizo za kale mchezo huu ulichezwa na askari wa
jeshi la China walioutumia mianzi kwa kuweka alama za magoli. Wale waliocheza
vizuri walipewa zawadi na baadhi yao
kupandishwa vyeo.
Lakini ole kwa wale waliocheza vibaya. Waliadhibiwa na
baadhi yao kuuawa. Huu ni ushahidi thabiti wa uhasama uliopindukia kwa wapenzi na
mashabiki (manazi).
Wajapan nao wanayo hadithi yao ya kale katika soka.
Wao waliuita mchezo wenye mithili ya kandada kwa jina la Kemari (haijajulikana
kaama ndio chimbuko la mchezo wa kamari).
Miaka kadhaa iliyofuata majirani zao China walianza
kucheza mechi za kirafiki lakini kumbukumbu hazionyeshi nani kati yao alikuwa
akilisakata kabumbu vizuri zaidi.
Huko Ugiriki, miamba ya zamani Warumi wao pia walikuwa
wakitaba sana kwa mchezo wa mpira ambao ulikuwa ukijulikana kama
Halic-Episykros.
Mfano wa mchezo huu wa mpira wa Kirumi ni sawa na ule
wa mabavu na mchezo wa raga (rugby) katika nyakati za sasa. Watu wa Florence na
Ufaransa nao walisema kuwa hakuwa nyuma kamwe katika kulisakata kandanda.
Nyaraka za historia na hadithi za maandishi
zinaonyesha vizuri kuwepo kwa kandanda maeneo hayo katika miaka mingi
iliyopita. Huko Florence mchezo huo ulikuwa ukijulikana kama Halic-Calcio jina
ambalo baadaye lilizagaa barani Ulaya katika karne ya 17.
Wakati huo Halic-Calcio ilikuwa burudani kubwa kwa
mwamwinyi na masikini. Lakini palikuwepo na tofauti kubwa kati ya mchezo huu wa
Halic-Calcio na kandanda la sasa.
Kwa mfano kulikuwa na wachezaji 27 wakati huo uwanjani
tofauti na ilivyo sasa ya wachezaji 11. Lakini lazima kulikuwa na vurugu
uwanjani tofauti na ilivyo sasa hali hiyo imedhibitiwa kwa kiasi kikubwa licha
ya mechi kadhaa kurudia tabia hiyo.
Nchini Uingereza nako ilikuwa ni mchezo mithili ya huo
katika miji ya Ashbourne, Derbyshire ambako kumekuwa na kumbukizi katika
milango ya Ukumbi wa Manispaa ya Ashford na milango ya kanisa lililopo jirani
kukumbushana dimba la hapo kale la soka.
Ilikuwa karne ya 16 wakati ambapo soka karibia upigwe
marufuku katika nchi kadhaa wakati wa vurumai na uhasama ulipojitokeza ambapo
usalama wa wachezaji na watazamaji yalikuwa hatarini. Hapo ndipo ikabidi baadhi
ya sheria zitungwe ili kulinda usalama wa wachezaji, waamuzi na watazamaji.
Lakini sheria hasa za kuongoza mchezo huo hazikutungwa
mpaka karne ya 19 katika mkutano wa kwanza wa soka uliofanyika nchini Uingereza
mnamo mwaka 1848.
Mojawapo ya sheria iliyotungwa na kupata ufafanuzi
wake ilikuwa ni kwa mchezaji, isipokuwa mlinzi, golikipa kutoruhusiwa mikono. Pamoja
na hiyo ikaja sheria ya Kuotea (Offside), kipengele ambacho hadi leo kimekuwa
kigumu na chenye kuleta mzozo mkubwa katika soka.
0 Comments:
Post a Comment