Mwalimu mmoja aliwahi kusema “Safari ya matembezi iliyopangwa
vizuri hunufaisha kwelikweli, ikipanua maoni ya mhusika na kumsaidia aweze
kujitegemea mwenyewe.”
Matembezi yanaweza kuhusisha rafiki zako au familia
yako au wewe mwenyewe binafsi. Basi, ufanye nini ukipata fursa ya kwenda kufanya
matembezi.
Kija Elias Kisena ni miongoni mwa wakazi wa mji wa
Moshi ambaye hufanya matembezi yake mara kwa mara katika maeneo mbalimbali
nchini.
Lakini safari hii alifanya matembezi katika mto
Karanga uliopo mjini Moshi karibu na daraja la Bonite ambako kumekuwa na
shughuli kubwa ya kuosha karoti katika mto huo.
Alichokifanya Kija ilikuwa ni kuzungumza na watu wale
na kikubwa zaidi katika matembezi yake ilikuwa ni kuchukua picha za ukumbusho.
“Nimefurahi kufanya matembezi hapa, hali ya hewa leo
ilikuwa nzuri sio ya jua na ubaridi kwa mbali nimejisikia furaha,” alisema
Kija.
Hivyo basi kuna mambo mengi ya kufanya unapofanya
matembezi lakini miongoni mwa mambo muhimu ya kuzingatia ni kutembea na kamera
kwa ajili ya kupiga picha matukio yote yanayofaa kwenye safari yako ya
matembezi.
0 Comments:
Post a Comment