Saturday, July 18, 2020

Paulo George Maile achukua fomu kuwania udiwani Soweto, Moshi


Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Soweto Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, kimewataka wanachama wanaochukua fomu za kugombea nafasi za Udiwani kuacha kuchafuana na badala yake wanapaswa kufuata kanuni na taratibu na endapo watakwenda kinyume na maelekezo hayo, watakuwa wamepoteza sifa ya kugombea.

Hayo yamesemwa jana na Katibu wa chama hicho Kata ya Soweto Severin Mrosso, wakati alipokuwa akimkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya Udiwani Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya PAMA Online Security, Paulo George Maile ambaye amekuwa miongoni mwa watia nia aliyejitokeza kugombea nafasi hiyo.

Mrosso amesema kuwa wanachama wanaohitaji kugombea nafasi hizo wanapaswa kufuata kanuni na taratibu kwani endapo wataenda kinyume na maelekezo hayo watakuwa wamepoteza sifa ya kugombea na muda utakapofika wasishangae kuona majina yao yamekatwa.

“Uchaguzi huu ni ndani ya CCM kwa ajili ya kumpata mgombea ambaye atakwenda kushiriki katika uchaguzi mkuu na vyama vingine, hivyo tunahitaji wagombea wote wawe na mshikamano na umoja kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu zilizopo kwani CCM kina misingi yake,”.

0 Comments:

Post a Comment