Hapo awali rais huyo aliupuuzia ugonjwa huo akiuuita
kuwa mafua kidogo, sasa hivi anaugua homa, kikohozi na maumivu ya misuli
kulingana na vyombo vya habari vya ndani.
Siku ya Jumatatu alionekana hadharani akiwa amevalia
Barakoa na kudaiwa kuwaeleza wafuasi wake kutomsogelea.
Rais Bolsonaro ambaye mara kwa mara amekuwa akikataa
kuvaa barakoa alisema pia amechunguzwa mapafu kwa kutumia kipimo cha picha cha
X-ray katika hospitali ya kijeshi kama tahadhari.
''Ninaepuka kuwakaribia watu, kwa sababu nimetoka
hospitali kupima COVID-19, lakini najisikia vizuri. Asilimia 90 ya watu
watakaoambukizwa hawatokuwa na dalili. Tunachopaswa kufanya ni kutovieneza
virusi kwa wengine. Iwapo nitaathirika virusi vya corona, sitokuwa na wasiwasi,
itakuwa ni sawa kama kuwa na mafua au homa. Tuheshimu miongozo ya Wizara ya
Afya,'' alifafanua Bolsonaro.
CHANZO: DW
0 Comments:
Post a Comment