Ota Benga alikuwa mwafrika mzaliwa wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo wakati huo ikifahamika kama koloni la Wabelgiji la Kongo.
Kijana huyu anakumbukwa kutokana na kile alichofanya
na kufanyiwa na wazungu. Ota Benga alizaliwa mnamo mwaka 1883 katika misitu ya
Kongo kwa jamii ya watu wa Bambuti. Jamii ya Bambuti ilikuwa ya mbilikimo.
Wazungu walipofika katika ardhi hiyo walikutana na
waafrika wakiendelea na maisha yao. Nao wakaanzisha muundo mpya wa maisha
ambapo miongoni mwa mambo wazungu waliyofanya ni kuwakamata wenyeji wa maeneo na
kuwafanya watumwa. Miongoni mwa waliokamatwa alikuwa Ota Benga.
Mnamo mwaka 1904 akiwa na umri wa 21 alisafirishwa
kutoka Kongo hadi nchini Marekani. Alipotua nchini Marekani alifikia huko St.
Louis, Missouri ambako kulikuwa na maonyesho ya biashara hususani maonyesho ya
wanyama yaliyokuwa yakifahamika kama Louisiana Purchase Exposition.
Benga alipekwa katika maonyesho ya wanyama mnamo mwaka
1906 ambapo wazungu walikuwa wakifika na kujifunza kwa watu wa aina mbalimbali
kutoka maeneo tofauti duniani. Benga alifikishwa Bronx Zoo jijini New York
ambapo watu mbalimbali walifika kumwona namna alivyokuwa.
Benga alifika nchini Marekani baada ya kuuzwa na
wafanyabiashara wa watumwa barani Afrika na mzungu aliyefahamika kwa jina la
Samuel Phillips Verner alimnunua kwa ajili ya kumpeleka kwenye maonyesho ya Watu wa Afrika nchini Marekani.
Hivyo wakati anaenda nchini Marekani aliambatana na Verner.
Alipofika katika Bustani ya Wanyama ya Bronx aliruhusiwa
kutembea katika bustani hiyo kabla ya kumweka pamoja na nyani katika bustani ya
nyani hao. Baada ya kuzuru kidogo nchini Marekani Verner akiwa na Benga
walifika katika maonyesho ya St. Louis na Benga akawa mtumwa huko Virginia
maisha yake yote hadi kifo chake akiwa na umri wa miaka 32.
Alifariki dunia Machi 20, 1916 kutokana na msongo wa mawazo ambapo aliamua kujiua kwa kujipiga risasi. Maisha yake nchini Marekani tangu siku ya kwanza alipofika magazeti ya Kiafrika ya nchini humpo yalikuwa yakipinga namna Benga alivyokuwa akitendewa.
Miongoni mwa waafrika waliosisimama kidete kupinga suala hilo ni Robert Stuart MacArthur ambaye alikuwa msemaji wa makanisa ya Wamarekani weusi alipeleka maombai yake kwa Meya wa Jiji la New wakati huo George B. McClellan Jr. kuhusu kuachiwa kwa Benga katika Bustani ya Wanyama ya Bronx.
Baadaye mwaka 1906 meya wa jiji hilo alimwachia Benga
baada ya kukaa miaka miwili bustanini hapo. Wakati anamwachia alimweka mikononi
mwa James M. Gordon ambaye alikuwa msimamizi wa makazi ya Yatima ya Howard
Colored mjini Brooklyn.
Mnamo mwaka 1910 Gordon alimpeleka Benga kuishi
Lynchburg huko Virginia ambako alikuwa
Benga alipewa nguo za Kimarekani aweze kuvaa na pia kubwa zaidi ni
kutokana na meno yake yaliyochongoka kama ya Simba. Kutokana na sifa hizo Benga
angeweza kukubalika kuishi na kupata uraia huko.
Ota Benga alianza kujifunza kiingereza na baada
alianza kufanya kazi katika kiwanda cha tumbaku cha Lynchburg. Akiwa hapo
alipata akili ya kurudi nyumbani kwao yaani barani Afrika lakini kutokana na
kuanza kwa Vita vya Kwanza vya Dunia mnamo mwaka 1914 meli zote hazikuruhusiwa
kusafirisha abiria yeyote.
Benga alipatwa na msongo wa mawazo kwani alikumbuka
sana nyumbani kwao hivyo kuona hivyo na mateso ya wakati huo nchini Marekani
aliamua kujiua kwa risasi mnamo mwaka 1916.
Benga akiwa miongoni mwa jamii ya watu wa Bambuti au
Mbuti alikuwa akiishi katika misitu ya Kiikweta karibu na mto Kasai ambapo
wakati huo lilikuwa ni eneo huru la Kongo. Watu wa jami yake walivamiwa na
jeshi la Publique lililopelekwa kwa amri ya Mfalme Leopold II wa Ubelgiji.
Madhumuni makubwa ilikuwa ni kumiliki eneo hilo
kijeshi na vyote vilivyomo ikiwamo watu ili waweze kutumika kwa ajili ya kilimo
cha mpira katika ardhi ya Kongo. Benga alikuwa na watoto wawili ambao waliuawa
wakati wa makabiliano na wanajeshi wa Kibelgiji, yeye peke alinusurika alikuwa
mwituni akiwinda wakati jeshi hilo lilipovamia kijiji chao.
Hatimaye alikuja kukamatwa na wafanyabiashara wa
watumwa waliokuwa wakifahamika kama Bashilele (Baschelel). Verner alimpata
Benga wakati alipokwenda katika kijiji cha Batwa alikowahi kuzuru awali kwa
ajili ya kupata watumwa na huko ndiko alikouziwa Benga.
Verner alimununua Benga kwa kilo ya Chumvi na kipande
kidogo cha nguo. Baadaye Verner alikaririwa alipofika nchini Marekani kwamba
alimchukua Benga baada ya kumnusuru kutoka katika mikononi mwa wanyama wakali.
Alikaa na Benga kwa takribani majuma mawili kabla ya kufika katika kijiji cha
Batwa.
Wanakijiji wa Batwa hawakuwa na imani na wazungu hata
kidogo ambapo wao walikuwa wakiwaita muzungu kwa maana kwamba ‘they developed
distrust for muzungu due to the abuses of King Leopold’s forces.’
Verner alipofika kijijini hapo hakufanikiwa kuwachukua
watu kuungana naye kwenda nchini Marekani hadi pale Benga alipowaambia watu wa
jamii yake kuwa muzungu ndiye aliyeokoa maisha yake na iliwezekana kumwamini
kutokana na Benga kuwa na mahusiano mazuri na wanakijiji wa Batwa.
Hivyo Verner aliwachukua wanaume wanne wa Kibatwa ili wamsindikize. Pia Verner alikuwa na waafrika wengine ambao hawakuwa mbilikimo. Watano kati yao walikuwa kutoka jamii ya watu wa Bakuba (Red Africans waliopo Kusini-Mashariki mwa DRC) akiwamo mtoto wa Mfalme Ndombe aliyekuwa mtawala wa Bakuba.
Benga alipowasili nchini Marekani alikuwa na uzito wa Kilo 58. Hata hivyo maisha yake yalikuwa ya taabu. Akiwa na umri wa miaka 32, mnamo Machi 20, 1916 aliazima bastola na kujipiga sehemu ya moyo baada ya kuona matumaini ya kurudi nyumbani hayapo.
Muda mchache kabla ya kujiua siku moja kabla ambayo
ilikuwa Machi 19, 1916 Benga ambaye wazungu walikuwa wakimwita Otto Bingo
alikusanya nyasi katika shamba kati ya nyumba aliyokuwa akiishi na majengo ya
seminari kisha akawasha moto.
Akatoa kofia aliyopewa awe anavaa iliyokuwa na mchoro
wa meno yalichongoka kisha akaanza kucheza, akiuzunguka moto huku akiimba nyimbo za huzuni na maombolezo
(zilijaa uchungu moyoni) kwa lugha ya Bambuti.
Kisha usiku ule ulipofika aliingia katika bohari ndogo
ya Mammy Joe katika mtaa wa Garfield.
Katika bohari hiyo alikuwa ameficha bastola
hiyo. Na mara baada ya watu kulala alijipiga risasi kwenye moyo na kufa
papo hapo.
Na ndio ukawa mwisho wa Ota Benga, kwani alifahamu
kuwa njia pekee ya kurudi katika ardhi yake ya asili hata kama kwa njia ya roho
ni kujiua. Kupelekwa kwake Lynchburg
kulikuwa na maana kubwa kwani ndio mahali pekee ambapo walau Ota Benga alipata
amani. Akiwa huko Benga alikutana na mwanamke mmoja anayechukuliwa kuwa ndiye
aliyemfundisha lugha ya Kiingereza Anna Spencer.
Anna Spencer alikuwa Mmarekani mweusi, mshairi alikuwa
akiishi katika mtaa wa Pierce na kufanya kazi katika Seminari na Chuo cha
Virginia.
Benga wakati alipokuwa akimaliza kazi za kiwandani alikuwa
akizama zake msituni kuwinda katika msitu mmoja unaofahamika kwa jina la
College Hill. Benga alikuwa akitumia upinde na mshale. Pia Benga ndiye
aliyemfundisha mtoto wa kiume wa Anne Spencer aliyefahamika kwa jina la
Chauncey namna ya kutumia upinde na mshale.
Alizikwa katika makaburi ya Old City huko Lynchburg,
Virginia katika eneo ambalo watu weusi walikuwa wakizikwa. Hapakuwa na alama
yoyote lakina alizikwa karibu na Gregory
W. Hayes (Hayes alikuwa kiongozi wa Jamii ya Wabaptisti Wamarekani Weusi huko
Richmond, Virginia alifariki mwaka Desemba 2, 1906; Huyu ni miongoni mwa walimpambania
Ota Benga kwani Hayes alitoa nafasi ya Benga kuishi na familia yake na kusoma
seminari.)
Vyanzo vya mdomo vinasema kwamba baadaye mabaki ya Hayes na Benga yalitolewa katika makaburi ya Old City na kuzikwa upya katika makaburi ya White Rock Hill ambayo baadaye yaliachwa ukiwa bila kuhudumiwa. Mnamo mwaka 2017 Ota Benga alikumbukwa huko Lynchburg ikiwa ni miaka 100 kupita.
0 Comments:
Post a Comment