Saturday, July 11, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Lady Bird Johnson ni nani?

Julai 11, 2007 alifariki dunia raia wa Marekani na mke wa Rais wa 36 wa taifa hilo Claudia Alta Taylor. Claudia alifahamika kwa jina la Lady Bird Johnson. Alikuwa first lady wa Rais Lyndon  B. Johnson. Pia alikuwa second lady wa Marekani kutoka mwaka 1961 hadi 1963.

Mwanamke huyo alifahamika sana kutokana na kuwa msomi mwanamke wa zama zake, alionyesha uwezo wake wa kusimamia na mwekezaji mwenye mafanikio makubwa.

Baada ya kuolewa na Lyndon mnamo mwaka 1934. Lyndon wakati huo alikuwa ni tumaini pekee la watu wa Austin, Texas.

Lady Bird alitumia elimu yake na uwezo wake wa kuongoza na kusimamia ofisi wakati Lyndon alipoenda katika jeshi la maji. Alinunua kituo cha redio na baadaye kituo cha televisheni ambavyo vyote kwa pamoja vilimpatia mapato na kumfanya Lyndon kuwa milionea.

Akiwa kama First Lady alivunja utaratibu uliozoeleka kwa kuingia moja kwa moja katika Bunge la Kongresi, pia alimwajiri Katibu Muhtasi wake mwenyewe na alikuwa muhimu katika harakati za uchaguzi nchini humo. 

Lyndon alikuwa muhimu katika kuandaa muswada wa kupendezesha miji na barabara kuu kwa kauli mbiu ya “Where flowers bloom, so does hope.”

Awali muswada huo ulikuwa ukifahamika kwa jina la Muswada wa Lady Bird, ambapo baadaye ikawa sheria ya Highway Beautification.

Lady Bird alitunukiwa Presidential Medal of Freedom Januari 10, 1977 na Rais Gerald Ford pia alitunukiwa Congressional Gold Medal ambazo hutunukiwa kwa wazalendo wa Marekani. 

Lady Bird alizaliwa Desemba 22, 1912 huko Karnack, Texas katika kaunti ya Harrison upande wa mashariki  karibu na Louisiana.

Alizaliwa katika nyumba ya matofali ya kuchoma ambapo baba yake aliinunua siku chache kabla ya yeye kuzaliwa. Mumewe alifariki dunia mnamo mwaka 1973 ikiwa ni miaka minne baada ya kumaliza vipindi vyake vya kuliongoza taifa hilo. Lyndon alifariki dunia kwa shambulio la moyo.

Lady Bird alikuwa kwenye mkutano na alipokuwa akimkaribia Lyndon alifariki dunia. Lady Bird aliratibu kila kitu kuhusu maziko yake siku iliyofuata na mwili wake ulilazwa katika nyumba yake ya milele siku mbili baadaye.

Lady Bird alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 94 kwa maradhi ya uzeeni. Mazisho yalihudhuriwa na watu wengi wakiwamo wanafamilia na Father Robert Scott wa Kanisa Katoliki.

0 Comments:

Post a Comment