Julai
10, 2019 alifariki mwigizaji wa kike wa Afrika Kusini Nomhle Nkonyeni.
Alifariki huko Port Elizabeth akiwa na umri wa miaka 77. Nyota huyo alianza
kuwika tangu miaka ya mwanzoni ya 1961 hadi kifo chake.
Nkonyeni
aliibuka katika kipindi ambacho Afrika Kusini ikiwa katika dimbwi la Ubaguzi wa
Rangi(apartheid), yeye na wenzake walitaka kubadilisha maisha ya watu kupitia
jukwaa la sanaahivyo wakakutana na Athol Fugard na kutengeneza Serpent Players.
Nkonyeni
aliwahi kuigiza katika tamthilia ya runinga kama Mzansi, Tsha Tsha na
2007mini-series Society pia katika filamu nyingi ikiwamo ya Of Good Report.
Alizaliwa New Brighton, Port Elizabeth mnamo Aprili 9, 1942.
Alifanikiwa
kuwa na watoto wawili wa kwanza ni wa kiume Tebogo Nkonyeni (Machi 27, 1966) na
mwingine wa kike Thabang Nkonyeni (Aprili 22, 1968 na akafariki Agosti 11,
2009). Binti yake huyo alipoteza maisha kwa kuuawa.
Nkonyeni
alifariki dunia kwa homa muda mfupi na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
alitangaza siku mbili za maombolezo maalum ya Jimbo (Special Provincial Funeral
Category) kutokana na mchango wake uliotukuka wa sanaa na utamaduni nchini
Afrika Kusini.
Waziri
wa Eastern Cape Oscar Mabuyane alikaririwa akisema, “ Alikuwa kiungo muhimu
katika kuhamasisha muungano wa kijamii. Hakika tunakubali mchango wake. Tuna
deni kubwa la kumpata mtu wa aina yake. Alicheza nafasi mbalimbali katika
mazingira magumu. Wakati mwingine alitumia sanaa yake kuwasilisha ujumbe na pia
alipambana na ukosefu wa haki hadi kuwepo kwa serikali ya sasa.”
Mnamo
mwaka 2016 alitunukiwa tuzo ya SAFTAs Lifetime Achievement. Pia mwaka 2018
alitunukiwa tuzo ya Mafanikio ya Maisha na Eastern Cape katika tuzo za
Utamaduni. Mwaka 2019 alipewa Order of Ikhamanga kutokana na mchango wake
kwenye sanaa na utamaduni. Katika mahali alipozaliwa huko New Brighton barabara
ya Aggrey ilipewa jina lake.
0 Comments:
Post a Comment