Uongozi wa Kanisa la Furaha
Tanzania (KLFT), kwa niaba ya waumini wake wote limetoa pole kwa familia,
ndugu, marafiki na watanzania wote kwa msiba huu mzito wa Rais mstaafu Benjamin
William Mkapa.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Furaha
Tanzania Jones Molla, ametuma salam za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Magufuli na Watanzania wote kwa msiba mzito wa Rais mstaafu wa awamu
ya tatu Benjamin Mkapa.
Askofu Molla alisema rais Mkapa
ameacha hazina kubwa ya maarifa, uzoefu na maono ambayo ni jukumu la Watanzania
kukusanya , kuelewa na kujifunza.
Molla alisema Rais Mkapa
atakumbukwa kwa mengi mema yale aliyoyasimamia na kuyapigania katika kipindi
chote cha uhai wake hivyo Watanzania hawana budi kuyaendeleza kwa manufaa ya
taifa. Huku akiwaalika wakristo kuendelea
kuishi na kuyaenzi mema yote aliyofanya.
Askofu Molla alisema ni vyema wakristo wakakubali kwamba kifo kimeumbwa na Mwenyezi Mungu hivyo kila mmoja ndio njia yake hiyo atakayoipitia kwani Miongoni mwetu kuna wagonjwa wa kiroho wanahitaji kulishwa na neno lako .
“Bwana tumekuja tuwatupu hatuna kitu, kitu pekee tulichonacho ni Imani zetu, tunaamini Bwana utatuhurumia, kanisa linatuita, linatualika kuzama katika maombi ya toba, sala na matendo ya upendo.
0 Comments:
Post a Comment