Sunday, March 1, 2020

Watanzania waonja tena machungu ya Kili Marathon 2020

Mshindi wa Kili Marathon 2020 kwa wanaume raia wa Kenya Kiplagat Onesmus Kiplimo 

Mshindi wa Kili Marathon 2020 kwa wanawake raia wa Kenya Lydia Wafula

Mbio maarufu na kongwe nchini za Kili Marathon zimefanyika jana mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ikishuhudiwa wanariadha wa Tanzania wakionja tena machungu ya kukosa taji la ushindi katika kilometa 42.

Kiplagat Onesmus Kiplimo kwa wanaume na Lydia Wafula kwa wanawake walitwaa taji la ushindi katika mbio hizo zilizokuwa zikitimiza miaka 18 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2003.

Kiplimo alitumia saa 2:16:56 akifuatiwa na wakenya wenzake Abraham Too (2:17:08), Bernard Kipchirchir (2:18:02) huku Wafula akitumia saa 2:47:05, aliyefuatiwa na wakenya wenzake Rosina Kiboino (2:53:15) na Joan Rotich (2:53:15).

Mtanzania  Jackson Makombe kwa wanaume ndiye pekee aliingia katika kumi bora akishika nafasi ya nane baada ya saa 2:21:14.

Aidha kwa wanawake Mtanzania Angel John alishika nafasi ya tano akitumia saa 3:00:33 akifuatiwa na Sara Ramadhani nafasi ya sita baada ya saa 3:03:48 na Banueli Brighton akishika nafasi ya saba baada ya saa 3:15:36

Viongozi wa kada mbalimbali walikuwapo katika mbio hizo akiwamo Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangalla, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira, Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Raymond Mboya na wengine wengi tu.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira (kushoto) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Raymond Mboya muda mchache kabla hawajaanza kukmbia mbio za kilometa 5.

Waziri wa Utalii na Maliasili Kigwangalla akiwa na Haji Manala muda mchache kabla ya kuanza kufuta vilima vya Tigo Kili Half Marathon 2020

STORY & PHOTO BY: Jabir Johnson
EMAIL: jabirjohnson2020@gmail.com

0 Comments:

Post a Comment