Machi 19, 1933 alifariki dunia mhamiaji wa Italia aliyepata uraia wa Marekani Giuseppe "Joe" Zangara alifanya jaribio la kutaka kumuua Rais wa 32 wa Marekani Franklin Delano Roosevelt.
Zangara alifanya jaribio siku 17 kabla ya kuapishwa kwa Rais Franklin kuwa kiongozi mkuu wa taifa hilo ambayo ilikuwa ni Februari 15, 1933.
Wakati wa hotuba ya usiku huko Miami, Florida Zangara alifyatua risasi tano kutoka katika bastola yake ambayo alikuwa amenunua siku chache kabla ya kufanya tukio hilo.
Hata hivyo katika jaribio hilo risasi hizo zilimkosa Roosevelt na kumvaa Anton Cermark ambaye alikuwa Meya wa Chicago.
Mnamo Februari 15, 1933 Roosevelt alikuwa akihutubia usiku nyuma ya gari ambalo lilikuwa wazi maeneo ya Bayfront Park huko Miamo Florida ambako Zangara alikuwa akifanya kazi zake ambazo zilikuwa zikimpatia ujira.
Wakati Zangara alikuwa amenunua bastola yake ambayo kwa wakati huo ilikuwa ikiuzwa dola nane za Kimarekani kwa sasa ingekuwa alinunua kwa shilingi laki nne za Kitanzania.
Kwa kimo Zangara alikuwa na futi 5 hivyo hakukuwa na uwezekano wa kuonwa na watu waliokuwa mbele.
Akiwa nyuma ya mwanamke aliyefahamika kwa jina la Lilian Cross aliyekuwa amevaa kofia pana ambayo ilimkinga asionekana kirahisi.
Alipotandika risasi ya kwanza mwanamke huyo na wengine walitaka kuidaka bastola hiyo, hapo ndipo alipowachabanga risasi wengine wanne jumla watu watano walipigwa risasi katika tukio hilo.
Mrs. Joseph H. Gill (alijeruhiwa vibaya); Miss Margaret Kruis wa Newark, N.J.; Bodigadi na mpelelezi wa New York William Sinnott; Russell Caldwell wa Miami; na Meya wa Chicago Anton Cermak,aliyekuwa anakimbia kumuokoa Roosevelt. Roosevelt hajeruhiwa katika tukio hilo; Gazeti la Trube liliandika kuhusu meya huyo wa Chicago kuwa alimwambia maneno haya, "I'm glad it was me, not you."
Zangara alizaliwa Septemba 7, 1900 huko Ferruzzano, Calabria nchini Italia.
Baada ya kuitumia Italia katika vita vya kwanza kwenye safu za milima ya Alps waliondoka na mjomba wake kwenda Marekani mwaka 1923.
Walipofika nchini Marekani walitua katika mji wa Paterson huko New Jersey na alipata uraia wa Marekani miaka sita baadaye yaani mwaka 1929.
Zangara alikuwa na elimu ndogo katika maisha yake ambayo ilimfanya awe mfyatua tofali na mjenzi wa nyumba za matofali (fundi ujenzi).
Hata hivyo katika maisha yake alikuwa na matatizo katika tumbo kwani mara kwa mara alikuwa akipata maumivu makali katika tumbo ambayo madaktari walimwambia kuwa maumivu hayo ni sugu na hayana tiba.
Mnamo mwaka 1926 alikwenda kuangalia lakini haikusaidia zaidi sana maumivu yalizidi. Hata hivyo baadaye iligunduliwa kuwa nyongo ilikuwa na matatizo.
Akiwa jela aliwahi kusema kuwa matatizo hayo yalitokana na baba yake ambaye alikuwa akimlazimisha kufanya kazi ngumu katika shamba katika umri mdogo.
Aliandika katika kumbukumbu zake kwamba maumivu hayo yalimuanza tangu akiwa na miaka sita.
Zangara alikiri akiwa katika jela ya Dade County Courthouse akisema, "I have the gun in my hand. I kill kings and presidents first and next all capitalists." Zangara alihukumiwa miaka 80 jela kwa makosa manne aliyokutwa nayo, Zangara alimwambia jaji wa Mahakama "Four times 20 is 80. Oh, judge, don't be stingy. Give me a hundred years."
Meya Chicago alifariki dunia siku 19 baadaye ambayo ilikuwa Machi 6, 1933 siku mbili baada ya Roosevelt kuapishwa rasmi.
Hata hivyo Zangara alikuja kuhukumiwa kifo na Jaji Uly Thompson. Baada ya Zangara kusikiliza hukumu hiyo alisikika akisema, "You give me electric chair. I no afraid of that chair! You one of capitalists. You is crook man too. Put me in electric chair. I no care!"
Ikumbukwe kwamba katika sheria za Florida aliyehukumiwa kifo hawezi kuchanganywa na wafungwa wengine.
0 Comments:
Post a Comment