Kocha
Swalehe Muhina wa Mbuyuni Market FC amesema kushindwa kupata matokeo hakujatokana
na kuchelewa kupasha mwili joto (warm up) isipokuwa Mungu alipanga yake.
Akizungumza
baada ya mchezo huo dhidi ya Muheza United wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa kituo
cha Kilimanjaro uliochezwa asubuhi ya Machi 14 mwaka huu uliochezwa katika
Uwanja wa Ushirika mjini Moshi amesema malengo ya ushindi hayakutimia ya kuanza
na ushindi ili kujiweka pazuri.
Hayo
yamejiri baada ya kocha Mousa Omary kujigamba kwa kuchelewa kwa Mbuyuni Market
FC kupasha mwili joto ndio ilikuwa sababu ya wao kutumia udhaifu huo kupata
matokeo katika mchezo wa kwanza.
“Unapocheza
na mwenyeji lazima umheshimu, sisi tuliwahi kufanya warm up na wao walichelewa
hivyo tukaambiana kuwa tupambane katika dakika 20 za mwanzo tupate bao na
tukafanikiwa,” alisema kocha Mousa.
Hata
hivyo kocha Mousa aliweka bayana kuwa hali ya uwanja haikuwa rafiki kutokana na
mvua hivyo hawakucheza kwa kujiachia sana zaidi ya kujilinda.
Mhina
ameweka bayana kuwa kila kitu anapanga Mungu na hivyo bahati haikuwa kwao,
isipokuwa mchezo ujao utakuwa wa damu na jasho kuhakikisha wanapata matokeo
mazuri.
“Inawezekana
hapa kupata nafasi ya kwenda daraja la pili, mechi ijayo ni damu na jasho kuhakikisha
tunafanya vizuri tuyasahau yaliyopita kwani yamepita kilichopo ni kuangalia
mbele,” amesema Mhina.
Kikosi
cha Mbuyuni Market kiliundwa na; Abed Dismas, Ambokile William, Peter Kimaro,
Wilson Nangu, George Malbiche, Swalehe Mohamed (C), Eliudi Mlambi, Shaban
Hassan, Hamad Hamad, Fadhil Kizenga, Tumaini Baraka.
Kikosi
cha Muheza United kiliundwa na; Ally Mattaka, Ibrahimu Salimu, Awadhi Thomas,
Abdul Mngota (C), Adam Rajabu, Emmanuel Haule, Kondo Shaibu, Ramadhani Msumi,
Abbasi Athumani, Hussein Iddi.
STORY
& PHOTO BY: Jabir Johnson
EMAIL:
jabirjohnson2020@gmail.com
DATE:
Machi 14, 2020
0 Comments:
Post a Comment