Machi 23, 2015 alifariki dunia mwanasiasa na mwanasheria wa Singapore Lee Kwan Yew. Mwanasiasa huyu alikuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Singapore akishikilia wadhifa huo kutoka mwaka 1959 hadi 1990.
Alikuwa akifahamika kwa kifupi kama LKY na katika miaka ya mwanzoni alikuwa akifahamika kwa jina Harry Lee kama ambavyo wapenzi na mashabiki wa mwanasiasa huyo walivyopenda kumwita.
Kutokana na kuwa miongoni mwa waanzilishi wa Chama cha People's Action, Lee alitambuliwa kama baba wa taifa hilo lililopo Kusini Mashariki ya bara la Asia.
Hiyo ilitokana na namna alivyoweza kuitoa nchi hiyo kutoka ulimwengu wa tatu na kuipeleka katika ulimwengu wa kwanza yaani kutoka kuwa nchi inayoendelea hadi nchi iliyoendelea.
Na aliyafanya hayo ndani ya kizazi kimoja chini ya uongozi wake. Lee Kuan Yew alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 91 kwa ugonjwa wa kichomi.
Serikali ya Singapore ilitangaza maombolezo ya wiki moja huku watu akali ya milioni 1.7 walitoa heshima zao za mwisho katika Bunge na maeneo mengine yaliyotengwa kwa ajili ya kumuaga kiongozi huyo.
Mnamo Novemba 6, 2011 binti wa mwanasiasa huyo Lee Wei Ling aliandika katika makala ya ke kwenye gazeti la Sunday Times kuwa baba yake alikuwa na maradhi ya neuropathy kwa upande wa nyuma wa neva za ubongo na uti wa mgongo ambazo zingemfanya ashindwe kutembea au kuhisi chochote.
Katika makala hayo Wei Ling aliweka bayana kuwa yeye ndiye aliyeongozana naye kukutana na Katibu Mkuu Kiongozi wa zamani wa Ikulu ya Marekani Henry Kissinger huko Connnecticut Oktoba 2009.
Mnamo Februari 15, 2013 Lee Kuan Yew alipelekwa Hospitali ya Singapore kutokana na kuendelea kusumbuliwa na damu kushindwa kufika vizuri katika ubongo ambapo ilikwenda sambamba na shambulio la moyo ambapo mapigo ya moyo yalikuwa hayaendi kama inavyotakiwa.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yake ya siasa alikosa Chakula cha Jioni cha kuupokea Mwaka Mpya wa Kichina ambao ulikuwa ukifanyika katika kitongoji cha Tanjong Pagar.
Katika tukio hilo Lee Kuan Yew alialikwa kama mgeni wa heshima.
Akiwa hospitali hapo aliendelea kupokea matibabu.
Mnamo Februari 2015 hali yake ilizidi kuwa mbaya na kuzua taharuki na uvumi miongoni mwa visa hivyo ilikuwa ni kutengenezwa kwa wavuti inayofanana na ofisi ya Waziri Mkuu na kutangaza kuhusu kufariki kwake kiongozi huyo hiyo ilikuwa Februari 18, 2015.
Siku tano baadaye Waziri Mkuu Lee Hsien Loong ambaye ni mtoto wa kwanza wa Lee Kuan Yew alitangaza kifo cha baba yake. Lee alisema baba ya alifariki dunia Jumatatu ya Machi 23 saa 3:18 asubuhi kwa saa za Singapore sawa na Jumapili ya saa 4:18 usiku nchini Tanzania.
Singapore ilipata uhuru wake na kuwa Jamhuri ya Singapore huku ikisalia kuwa katika Jumuiya ya Madola mnamo Agosti 9, 1965 na Lee Kuan Yew alikuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa taifa hilo huku Yusof bin Ishak alitawazwa kuwa Rais.
Mnamo mwaka 1967 Singapore ilikuwa miongoni mwa mataifa yaliyounda Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki kwa Asia (ASEAN).
Hata hivyo iljiondoa mnamo mwaka 1969 huku Lee Kuan Yew akiweka msisitizo katika ukuaji wa haraka wa kiuchumi, kuunga mkono ujasiriamali wa kibiashara.
Pia Lee Kuan Yew aliweka mipaka katika demokrasia ya ndani.
Hatua hiyo ilimsaidia sana kuitengeneza Singapore katika nusu karne iliyofuata na taifa hilo likapaa kutoka ulimwengu wa tatu hadi kuwa ulimwengu wa kwanza.
Mafanikio makubwa ya kiuchumi kwa taifa hilo yaliendelea katika miaka ya 1980 ambapo anguko la ajira lilipungua kutoka asilimia 3 na Pato la taifa lilifikia wastani wa asilimia 8 hadi mwaka 1999. Miaka ya 1980 Singapore ilianza kupanda katika viwanda vya teknolojia. Lee Kuan Yew alifanya hivyo ili kuweza kushindana na nchi jirani.
Uwanja wa Ndege Singapore Changi ulifunguliwa mwaka 1981 na Singapore Airlines. Bandari ya Singapore ilikuja kuwa kitovu cha biashara na miongoni mwa bandari ambazo muda iko busy.
Pia utoaji wa huduma nchini humo na utalii vilikuwa wakati wa utawala wa Lee Kuan Yew. Singapore ikaja kuwa kitovu cha usafirishaji na biashara na kitovu cha utalii.
Kuna wakati Lee Kuan Yew alichukuliwa kuwa ni mkandamizaji wa demokrasia ya Singapore lakini aliwajibu wakosoaji wake kuwa hakuna namna nyingine ya kumwongoza mtu mwenye asili ya China bila kumbana na alisisitiza kuwa yeyote atakayeinua kidole chake atakiona cha mtema kuni.
Katika mahojiano na CNN mwaka 1998 Kuhusu maoni yake kwa mashoga na wasagaji katika taifa lake Lee Kuan Yew alisema sio jukumu lake kukataza mapenzi ya jinsia moja isipokuwa ni jukumu la jamii yake kukubaliana au kutokubaliana na hilo na Lee aliongeza kuwa hawezi kuingilia kati uhusiano huo kwa namna yoyote ile.
Mnamo mwaka 2013 Lee Kuan Yew wakati wa mahojiano maalumu aliulizwa suala la dini yake, kiongozi huyo wa zamani wa Singapore alisema kuwa yeye sio Mkristo wala Mtao bali ni Mbuddha. Mara kadhaa alikuwa akijipambanua kuwa yeye ni Mbuddha.
Wazazi wake walikuwa wameelimika ambapo wakati anazaliwa walimpa jina la Kuan Yew wakiwa na maana ya 'Nuru na Mwangaza' hata hivyo haikuishia hapo babu yake upande wa baba yake alimwita Harry
Lee Kuan Yew alioa Septemba 30, 1950 mwanamke aliyefahamika kwa jina la Kwa Geok Choo. Lugha ya kwanza kwa wote wawili ilikuwa Kiingereza, mnamo mwaka 1955 alianza kujifunnza kichina akiwa na umri wa miaka 32.
Wakati wa Vita vya pili vya Dunia alijifunza Kijapan ili iweze kumsaidia kuishi na kwa kufanya hivyo alifanikiwa kuwa Mkalimani wa Kijapani wakati wa Utawala wa Japan nchini Singapore.
Lee na Kwa alifanikiwa kuzaa watoto wawili wa kiume na mmoja wa kike. Mtoto wake wa kwanza anafahamika kwa jina la Lee Hsien Loong ambaye ni Brigedia Jenerali mstaafu ambapo mwaka 2004 alikuja kuwa Waziri Mkuu wa Singapore.
Mnamo mwaka 2010 Lee Kuan Yew alikaririwa akisema, "I'm not saying that everything I did was right, but everything I did was for an honourable purpose. I had to do some nasty things, locking fellows up without trial."
kwa tafsiri ya kiswahili; "Sisemi kwamba kila kitu nilichofanya kilikuwa sawa, lakini kila kitu nilifanya ni kwa sababu ya heshima. Ilibidi nifanye vitu vibaya, kuwafungia wenzangu bila kesi."
0 Comments:
Post a Comment