Thursday, March 12, 2020

Epuka kufanya makosa katika malezi ya mtoto



Malezi ya watoto ni suala nyeti, pana, gumu, na lenye changamoto nyingi; hivyo linahitaji umakini mkubwa na maarifa stahiki.
Kutokana na umuhimu huu basi, ni wazi kuwa changamoto au matatizo mengi ya kimalezi yanayotokea kwenye maisha ya watoto yanatokana na makosa yanayofanywa na wazazi katika malezi.
Pamoja na kwamba hakuna kanuni ya malezi, lakini yapo makosa ambayo wazazi wanapaswa kuyaepuka katika swala la malezi ili kuhakikisha watoto wao wanakuwa katika maadili na misingi sahihi.
Yafuatayo ni mambo ambayo mzazi au mlezi anatakiwa kuyaepuka katika malezi ya kilasiku ya watoto.
1.   Kumfurahisha mtoto
2.   Kumwabudu mtoto
3.   Kujadili na kudharau wazazi na watoto wa wengine
4.   Kuwafundisha kuishi kwa sheria
5.   Kuwalazimisha kushika imani kwa lazima
6.   Kukosa muda wa kuwasikiliza
7.   Kugombana mbele ya watoto
8.   Kuruhusu tamaduni mbaya za jamii nyingine
9.   Kuwa mkatili kwa mtoto
10.                Kumfanyia mtoto kila kitu
11.                Kushindwa kumwandaa mtoto kwa ajili ya maisha ya baadaye
12.                Kushindwa kutawala ulaji wa mtoto
13.                Kushindwa kumfundisha elimu ya jinsia
14.                Kushindwa kuheshimu utu wake
 CHANZO: FAHAMU HILI


0 Comments:

Post a Comment