Machi 18, 1982 alifariki dunia Kamanda wa Jeshi la Kisovieti la Urusi Vasily Ivanovich Chuikov.
Alikuwa Kamanda wa 62 wa Jeshi hilo la Kisovieti ambaye aliongoza mapambano katika Vita ya Stalingard. Chuikov aliongoza mapambano makali kushuhudiwa katika vita vya pili vya Dunia.
Agosti 23, 1942 hadi Februari 2, 1943 takribani miezi saba ya mapambano hapo Stalingard kulishuhudiwa Majeshi ya Ujerumani yakipambana na Majeshi ya Usoviet katika mji wa Stalingard ambapo kwa sasa mji huo unafahamika kwa jina la Volgograd, uliopo Kusini mwa Russia.
Chuikov alishuhudia mapambano hayo ambapo takribani watu milioni mbili waliuawa, walijeruhiwa au kutekwa ikiwa ni rekodi ya juu katika vita hapa ulimwenguni.
Mapambano ya askari wa miguu, mapambano ya angani yalishuhudiwa katika vita hivyo ambapo Ujerumani ilishindwa kufurukuta na ikabidi ikimbie kuelekea upande wa Magharibi ikiwa ni mpango wa kujiepusha na hatari zaidi kwani vita hivyo mjini Stalingrad havikuwa vya kawaida.
Baada ya vita vya Pili vya Dunia Chuikov alikuwa Mkuu wa Vikosi nchini Ujerumani kutoka mwaka 1949 hadi 1953.
Pia Chuikov alikuwa Kamanda wa Mkoa wa Kijeshi wa Kiev kutoka mwaka 1953 hadi 1960.
Haikutosha alipewa tena kusimamia Mkuu wa Vikosi vya Usalama wa Kisoviet na Naibu Waziri wa Ulinzi kutoka mwaka 1961 hadi mwaka 1972.
Haikutosha enzi za uhai wake Chuikov aliwahi kutunukiwa medali mbalimbali ikiwamo ya Shujaa wa Umoja wa Kisoshalisti wa Kisoviet (USSR) mara mbili mwaka 1944 na mwaka 1945.
Pia alitunukiwa tuzo ya Huduma iliyotukuka wakati wa Vita vya Stalingrad aliyopewa na Marekani. Mnamo mwaka 1955 alitajwa kuwa Field Marshal wa Kisovieti.
Chuikov alizikwa katika eneo la Kumbukumbu ya Stalingrad katika kitongoji cha Mamayev Kurgan.
Katika eneo hilo la Mamayev Kugan wakati wa Vita vya Stalingrad ndiko kulikoshuhudiwa mapambano makali zaidi katika vita hivyo vya miezi saba.
Familia yake ilitoa taarifa hiyo kuwa Jenerali wa Vikosi vya Kijeshi aliyeongoza mapambano makali kuwhai kutokea katika vita vya Pili vya Dunia amefariki dunia.
Wakati Chuikov anafariki dunia, alikuwa amesalia Jenerali mwingine waliyeongoza naye mapambano katika vita vya Stalingrad Ivan Khristoforovich Bagramyan wakati huo akiwa na miaka 84 ambaye alifariki miezi sita baadaye Septemba 2, 1982.
Ilielezwa kuwa wakati wa uongozi wake katika vita ya Stalingrad Chuikov aliwaambia wanajeshi wake kuwa ni lazima waushikilie mji huo au wafie hapo.
Wanajeshi wa Kisovieti akali ya 400,000 walipoteza maisha na zaidi ya wanajeshi 300,000 wa Kijerumani walikufa katika vita hiyo ya Stalingrad.
0 Comments:
Post a Comment