Machi 19, 1976 alizaliwa mwanasoka wa kimataifa wa Italia Allesandro Nesta. Nyota huyo aliwahi kutwaa tuzo ya mlinzi bora wa Ligi Kuu ya Italia Seria A mara nne.
Alizaliwa jijini Rome. Nesta aligunduliwa kuwa na kipaji cha soka na Francesco Rocca ambaye alikuwa skauti wa vipaji wa Roma, lakini baba yake alikuwa shabiki mkubwa wa klabu ya Lazio hivyo akaipiga chini ofa ya mwanaye kwenda Roma.
Alianza maisha yake ya soka na Lazio mnamo mwaka 1985 akicheza katika nafasi mbalimbali alipokuwa dimbani.
Alihudumu katika nafasi ya ushambuliaji na kiungo kabla hajaweka katika nafasi ya ulinzi.
Msimu wa 1993-94 aliitwa katika kikosi cha wakubwa na mchezo wake wa kwanza ulikuwa Machi 13, 1994 dhidi ya Udinese ambao ulimalizika kwa sare ya 2-2.
Siku hiyo Nesta aliingia katika dakika ya 78 akichukua nafasi ya Pierluigi Casiraghi.
Mnamo mwaka 1997 alipewa unahodha wakati huo kocha Sven-Goran Eriksson ambapo aliisaidia Lazio kutwaa taji la Coppa Italia mwaka 1998 dhidi ya Milan katika fainali. Katika mchezo huo alifunga bao la ushindi.
Msimu huo ilishindikana kutwaa taji la UEFA lakini Lazio ilipoteza dhidi ya Inter Milan. Nesta alitunukiwa tuzo ya Mchezaji Chipukizi wa Mwaka wa soka la Italia lutokana na kiwango bora alichokionyesha msimu huo.
Baada ya kuingoza Lazio katika mafaniko ya Coppa Italia pia aliiongoza kutwaa taji la Washindi mnamo mwaka 1999.
Mwaka 2000 aliiongoza kutwaa Coppa Italia kwa mara nyingine ikiwa ni rekodi nzuri klabu hapo kama ile ya mwaka 1974.
Msimu huo ilishuhudiwa Nesta akishinda tuzo nne mfululizo za mlinzi bora wa mwaka.
Katika majira ya joto ilishuhudiwa Nesta kaitua zake Milan kwa kitita cha Euro milioni 31.
Kwa misimu 10 alishinda mataji likiwamo la Skudetto mwaka 2004 na 2011; pia Coppa Italia mwaka 2003.
Pia Nesta aliytwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2003 na 2007 na mwaka 2007 alitwaa taji la klabu ya Dunia (FIFA Club World Cup).
Katika timu ya taifa alihudumu katika mechi 78 kutoka mwaka 1996 hadi 2006 huku akiikosa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2006 kutokana na majeruhi.
Aliondoka Milan mwaka 2012 na kwenda zake Amerika ya Kaskazini katika klabu ya Montreal Impact Pia alikwenda kuhudumu na Chennaiyin ya India kwa msimu mmoja kabla hajastaafu mwaka 2014.
Kutoka hapo aliingia katika masuala ya menejimenti katika klabu ya Miami kwa misimu miwili mwaka 2016 na 2017.
Pia msimu wa 2018-19 aliisimamia Associazione Calcistica Perugia Calcio iliyopo Serie B na kutoka mwaka 2019 hadi sasa yupo na klabu ya Frisnone iliyopo Serie B.
0 Comments:
Post a Comment