Monday, March 9, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: The Notorius B.I.G ni nani?

Machi 9, 1997 alifariki dunia mtunzi wa nyimbo, mwigizaji na rapa wa Marekani Christopher George Latore Wallace maarufu The Notorius B.I.G Mnamo Februari 1997 Wallace alisafiri kwenda California kwa ajili ya kupigia promo 'Life After Death' yaani maisha baada ya kifo na singo aliyorekodi ya Hypnotize. 

Machi 5 alifanya mahojiano na The Dog House katika kituo cha redio  KYLD huko San Francisco. Katika mahojiano hayo Wallace alisema amekodi watu kwa ajili ya ulinzi kwani usalama wa maisha yake ulikuwa mashakani. 

Machi 8, 1997 Wallace alikuwa akimkabidhi msanii Toni Braxton tuzo yake katika toleo la 11 la sherehe za Soul Train Music zilizofanyika Los Angeles. 

Baada ya hapo alikwenda zake kula bata katika hafla iliyoandaliwa na Vibe and Qwest Records katika Makumbusho ya Petersen Automotive. 

Saa 12:45 asubuhi mitaa ilikuwa imefurika watu waliokuwa wakiondoka katika sherehe hiyo. Gari lililokuwa limembeba Wallace lilisimama katika taa za kuongozea magari na waenda kwa miguu ikiwa ni mita 46 kutoka Petersen Automotive, gari nyeusi aina ya Chevy Impala ilijivuta karibu na usawa wa gari la Wallace. 

Dereva wa Impala ambaye hakujulikana lakini ni Mmarekani mweusi akiwa katika suti ya bluu na tai alikaribia dirishani alipokaa Wallace na kutoa bastola ya rangi ya bluu na kuielekeza alipokaa Wallace. 

Risasi nne kutoka katika bastola hiyo zilimtandika Wallace ambaye alikimbizwa katika hospitali ya Cedars-Sinai na ilipofika saa 1:15 ilitangazwa kuwa Notorius B.I.G amefariki dunia. Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 24. 

Sababu za mauaji hayo ni ugomvi kati yake na Tupac Amar Shakur ambaye alifariki miezi sita kabla ya Notorius B.I.G Miaka 15 baadaye uchunguzi zaidi ulifanyika na ulionyesha kuwa risasi ya mwisho ilikuwa mbaya zaidi kwani iliingia kupitia paja la kulia na uliharibu utumbo mnene, ini, moyo na pafu la kushoto kabla ya kukwama katika bega lake la kushoto. 

Ibada ya mazishi ya ilifanyika katika viunga Frank E. Campbell huko Manhattan Machi 18, 1997. 
Waombolezaji akali ya 350 walihudhuria wakiwamo Lil' Cease, Queen Latifah, Flava Flav, Mary J. Blige, Lil' Kim, Run–D.M.C., DJ Kool Herc, Treach, Busta Rhymes, Salt-N-Pepa, DJ Spinderella, Foxy Brown, and Sister Souljah. Mwili wake ulichomwa moto na majivu yalikabidhiwa kwa familia yake. 
Katika ugomvi wake na kambi pinzani ya West Coast. Kw amara ya kwanza wawili hawa walikutana Los Angeles na urafiki wao ukaanzia hapo lakini baadaye uligeuka shubiri hadi umauti wao na wawili hao ndio waliotengeneza kambi mbili ya East Coast na West Coast. 

Notorius alikuwa wa East Coast kwani alizaliwa Brooklyn katika viunga vya jiji la New York na kukulia humo. Kwenye wimbo wa Notorius wa "Who shot ya", kuna mstari unasema, "Come here..come here...open your fucking mouth...Didn't I tell you not to fuck with me?...cant talk with a gun in your mouth huh? Bitch ass nigga,what.(Kwa kifupi ilitafsiriwa kwamba alikuwa akimuimbia Tupac kuhusu tukio la kupigwa risasi kwake.

Katika wimbo wa Tupac, "Hit em up", kuna mstari unasema, "who shot me, but punks didn't finish now you are about to feel the wrath of a manace nigga. I hit em up!"(Unaweza ukaona ni mistari iliyokaa wazi kama jibu la moja kwa moja kwa nyimbo ya "who shot ya".)

Miaka ya mwishoni 1995 mpaka mwanzoni 1996 Tupac alitoa mfululizo wa nyimbo nyingi zikimlenga kumtukana, kumtishia na kumdhalilisha Notorious BIG, Bad boy records na wasanii wote waliokuwa chini ya lebo hiyo. 

Mfano nyimbo kama "Against all odds", "Bomb first" na "Hit em up".

Notorious BIG naye hakuwa nyuma kwani aliachia nyimbo iliyoitwa, "Long kiss goodnight" ambayo mashairi yake yalionekana kumlenga Tupac na hata memba mmoja wa Bad Boy Records aitwaye Lil cease akihojiwa na jarida la XXL alikiri kuwa nyimbo hiyo ilimlenga Tupac ingawa bosi wa Bad boy, Puffy daddy, alikanusha mara moja akisema nyimbo hiyo haikumlenga Tupac, na kudai kama Notorious akitaka kumuimba Tupac basi angemtaja moja kwa moja na sio kuuma maneno.

Katika kipindi hicho vyombo vya habari viliripoti sana matukio haya na kwa kiasi kikubwa vilishiriki kuzidi kuchochea uhasama zaidi baina ya pande hizo mbili na hivyo kusababisha sasa hadi mtaani mashabiki kujitenga kwa kuchagua upande wa kushabikia hivyo uhasama ukahamia pia kwa mashabiki.

Septemba 13, 1996, Tupac alifariki dunia baada ya kushambuliwa kwa risasi akiwa kwenye gari siku sita nyuma, alipokuwa akitoka kuangalia pambano la ngumi la Mike Tyson, huko Las Vegas, Nevada.
Mwandishi mmoja aitwaye Chuck Philips aliandika kwenye makala moja iliyokuwa na kichwa cha habari,"Who killed Tupac Shakur", kuwa shambulio hilo lilifanywa na kundi moja la kihuni la Compton lijulikanalo kama South side crips, kulipiza kisasi cha mwenzao mmoja ambaye alipigwa na Tupac masaa kadhaa nyuma kabla ya shambulio hilo. 

Memba huyo aliyejulikana kama Orlando Anderson alikamatwa na polisi wa Las vegas na kuhojiwa mara moja tu kabla ya kuachiwa huru. 

Siku chache tu baada ya kuachiwa huru, Orlando Anderson aliuawa kwa risasi katika mapigano ya makundi mawili ya kihuni.(Inahisiwa hilo kundi jingine likuwa supporters wa Tupac, ni kama walienda kulipa kisasi na wao).

Mpaka leo hii mauaji hayo yamebaki kuwa hayajulikani kuwa yamefanywa na nani, ingawa wengi wanaamini Suge Knight anahusika kutokana na mlolongo wa matukio ulivyo.

Baada ya vifo hivyo, uhasama nao ukaoungua kwa kiasi kikubwa kama sio kwisha kabisa.

Notorious B.I.G alikulia Brooklyn, mji wa New York City, Wallace amekua kwenye kipindi cha matatizo ya uigaji tabia chafu kwenye miaka ya 1980, hivyo basi akaanza kujishughulisha na uuzaji haramu wa dawa za kulevya akiwa bado bwana mdogo kabisa. 

Wakati Wallace alitoa albamu yake ya kwanza mnamo mwaka 1994 'Ready to Die,' wakati huo alikuwa umbo la kati kwenye uwanja wa East Coast hip hop na kipindi hicho wasanii wa West Coast tayari walikuwa maarufu kwenye nyanja kuu za hip hop. 

Alizaliwa kwenye Hospitali ya St. Mary, ingawa inadaiwa kwamba alikulia mjini Bedford-Stuyvesant sehemu ya Brooklyn, nyumba ambayo Wallace alikulia ipo karibu na Clinton Hill. 

Wallace alikuwa mtoto pekee wa Voletta Wallace, mwalimu wa shule ya vidudu mwenye asili ya Jamaika, na George Latore, fundi wa kuchomelea na mwanasiasa wa muda mfupi wa Kijamaika. Baba yake aliiacha familia wakati Wallace akiwa na umri wa miaka miwili. 

Alipewa jina BIG kutokana na kwamba alikuwa na umbo kubwa kabla hajafikisha miaka 10. Darasa alikuwa mahiri katika somo la Kiingereza.

Akiwa na umri wa miaka 12, alianza kuuza dawa za kulevya. Mama yake, kutokana na kubanwa na kazi hakufahamu mara moja tabia ya Wallace hadi alipokuwa mtu mzima.


0 Comments:

Post a Comment