Monday, March 16, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Frank Sinatra ni nani?

Machi 16, 2016 alifariki dunia mwanamuziki, mwigizaji, na prodyuza wa Marekani Francis Albert Sinatra. 

Sinatra alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 82 kutokana na maradhi ya moyo Mei 14, 1998. Alifariki dunia mbele ya mkewe katika kituo cha afya cha Cedars-Sinai jijini Los Angeles.

Afya ya Sinatra katika maisha yake ilianza kuteteleka kwani alikuwa akipelekwa hospitalini mara kwa mara kutokana na kushindwa kupumua vizuri, shinikizo la damu, pneumonia na kansa ya kibofu hatimaye alipatikana na maradhi ya dementia ambayo hufanya uwezo wa kufikiri kupungua.

Katika karne ya 20 Sinatra alikuwa maarufu na aliweka rekodi ya kuwa miongoni mwa wasanii waliouza sana kazi zao ulimwenguni. 

Zaidi ya milioni 150 za kazi zake ziliingia sokoni ulimwenguni. Ni mzaliwa kutoka kizazi cha wahamiaji kutoka nchini Italia. 

Alizaliwa mjini Hoboken huko New Jersey. Sinatra alianza kuimba akiwa na Harry James na Tommy Dorsey waliokuwa viongozi wa bendi kati ya mwaka 1933-1947.

Mnamo mwaka 1943 alisaini kufanya kazi na Columbia Records, ambapo alikuwa nembo ya bobby soxers. 

Aliachia albamu ya kwanza mnamo mwaka 1946 aliyoipa jina la ‘The Voice of Frank Sinatra’  Mwanzoni mwa miaka ya 1950 alienda zake Las Vegas kwa ajili ya kujiimarisha. Akiwa huko mnamo mwaka 1953 alipata umaarufu zaidi kupitia albamu yake ya ‘From Here to Eternity’ ambayo ilimpa tuzo ya Oscar na ile ya Golden Globe. 

Hakuishia hapo pia alitoa albamu nyingine kama In the Wee Small Hours (1955), Songs for Swingin' Lovers! (1956), Come Fly with Me (1958), Only the Lonely (1958) na Nice 'n' Easy (1960). 
Sinatra aliachana na Capitol na kuanzisha lebo yake ya Reprise Records ambapo alifanikiwa kuachia albamu zilizompa mafanikio makubwa. 

Mnamo mwaka 1965 alitoa ‘September of My Years’ ambayo ilimpa tuzo ya Emmy. Albamu nyingine kama ‘Sinatra at the Sands’ aliyorekodia katika Sands Hotel and Casino mjini Las Vegas. 
Katika filamu aliigiza katika The Manchurian Candidate (1962) kabla ya hapo alionekana katika The Man with the Golden Arm (1955). 

Pia Sinatra alijihusisha na siasa katikati ya miaka 1940 alianza na kuwa miongoni mwa waliomfanyia kampeni za Urais Harry S. Truman, John Fitzgerald Kennedy na Ronald Reagan. Pia Sinatra alishawahi kuhojiwa na shirika la upelelezi la Marekani FBI kuhusu uhusiano wake na kundi la Mafia. 

Katika muziki Sinatra hakuwa kufundishwa kusoma muziki lakini alikuwa na uelewa mkubwa katika muziki na alijituma tangu akiwa mdogo ili kufanikiwa katika medani hiyo. 

Sinatra alizaliwa  Desemba 12, 1915 katika ghorofa katika mtaa wa 415 Monroe huko New Jersey kutoka kwa wazazi wahamiaji wa Kiitaliano  Natalina Dolly Garaventa na Antonio Martino Marty Sinatra. 

Wakati anazaliwa alikuwa na uzito wa kilo 6.1 ambapo alizaliwa kwa msaada wa vifaa maalumu vya uzalishaji ambavyo vilileta madhara katika maisha yake kwani shavu la kushoto lilipinda, shingo na sikio yalipata madhara. 

Ngoma ya siko lake la kushoto ilikuwa changamoto maisha yake hadi kifo chake. Kutokana na majeruhi hayo wakati anazaliwa ubatizo wake ulicheleweshwa katika Kanisa la Mt. Francis huko Hoboken hadi Aprili 2, 1916.

0 Comments:

Post a Comment