Tuesday, March 31, 2020

Ndugu wa Aliyefariki kwa Corona Mloganzila azungumza


Ndugu wa mtanzania aliyekufa kwa ugonjwa wa Corona  amesema mdogo wake, Iddy amefariki kwa ugonjwa wa corona leo alfajiri ya Machi 31, 2020 katika kituo cha matibabu ya wanaougua ugonjwa huo kilichopo Hospitali ya Mloganzila, Dar es Salaam. 

Ameeleza hayo leo wakati akizungumza na Mwananchi kuhusu taarifa za msiba huo. Iddy ni Mtanzania wa kwanza kufariki dunia kwa ugonjwa huo nchini.

Taarifa ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto iliyotolewa na Waziri Ummy Mwalimu imethibitisha kifo hicho na kubainisha kuwa alikuwa akipatiwa matibabu katika kituo hicho.

"Marehemu ni Mtanzania mwanaume mwenye umri wa miaka 49 ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine. Tunamuomba Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, na tunatoa pole kwa familia, ndugu jamaa wa marehemu, ilisomeka taarifa ya Waziri Ummy.

Amesema hadi sasa watu 19 wameambukizwa corona, aliyepona ni mmoja na kifo ni kimoja. Jana, Ummy alieleza kuwa kuongezeka kwa wagonjwa watano wa corona wakiwamo wawili waliokuwa wakifuatiliwa na kufanya idadi ya waliobainika kuwa na maambukizi nchini kufikia 19. 

Amesema mgonjwa wa pili ni mwana mke mwenye miaka 21 Mtanzania ambaye ni miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatiliwa. Kuhusu mgonjwa wa tatu, Ummy amesema ni mwanaume mwenye umri wa miaka 49 Mtanzania ambaye pia ni miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatiliwa.


0 Comments:

Post a Comment