Machi 31, 1980 alifariki dunia mwanariadha wa
kimataifa raia wa Marekani Jesse Owens. Jina lake halisi ni James Cleveland.
Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 66 huko Tucson
Arizona kwa ugonjwa wa saratani ya mapafu. Jesse Owens alianza uvutaji wa
sigara akiwa na umri wa miaka 32 na inaelezwa kwa siku alikuwa anavuta pakiti
moja.
Kwa miaka 35 tangu wakati huo alikuwa akivuta sigara.
Mnamo Desemba 1979 alipelekwa hospitalini ambako alilazwa kuanzia hapo alikuwa
akienda na kutoka kutoka na maradhi hayo. Alifariki dunia akiwa amezungukwa na
mkewe pamoja na wanafamilia wengine.
Jesse Owens alizikwa katika makaburi ya Oak Woods yaliyopo Chicago. Japokuwa Rais Jimmy Carter
alipuuzia maombi ya Owens kuhusu mgomo wa Olimpiki lakini kiongozi huyo wa
zamani alitoa rambirambi zake akisema, “Inawezekana hakuna mwanariadha
aliyekuwa nembo ya mapambano dhidi udhalimu, umaskini na ubaguzi wa rangi kama
Jesse Owens.” Jesse Owens alikuwa mwanariadha wa mbio za uwanjani maarufu track
and field.
Aliweka rekodi ya kutwaa medali nne katika michuano ya
Olimpiki ya mwaka 1936 iliyofanyika mjini Berlin katika Ujerumani ya Kinazi
iliyokuwa chini ya Adolf Hitler. Owens alikuwa mahiri katika kukimbia na miruko
ya chini.
Enzi zake alijulikana sana na alichukuliwa kuwa ni
mwanariadha mkubwa na maarufu katika historia yam bio za uwanjani. Aliweka
rekodi tatu za dunia chini ya saa moja kwenye tukio la mbio la mwaka 1935
lililofahamika kwa jina la Big Ten Track
lililofanyika Ann Arbor huko Michigan. Katika tukio hilo lilifahamika kama “The Greatest 45 minutes ever in sport.”
Owens alishinda medali nne katika michuano ya Olimpiki
mjini Berlin katika mita 100, mita 200, miruko ya chini na mbi za vijiti mita
100. Huyu ni mwanariadha aliyefanikiwa sana katika michuano hiyo na pia kama
mtu mweusi.
Kutokana na kuonyesha uwezo huo alitunukiwa heshima
iliyokuwa inatolewa na Adolf Hitler ya Aryan Supremacy licha ya kwamba hakuweza
kualikwa katika ikulu ya Ujerumani kushikana mkono na Hitler.
Pia katika kutambua mchango wake nchini Marekani kuna tuzo ya Jesse Owens kwa wanariadha
wanaofanya vizuri katika mbio za uwanja ambayo hutolea kila mwaka.
ESPN ilimweka katika nafasi ya sita katika wanamichezo
wakubwa katika Amerika ya Kaskazini waliowika kwenye karne ya 20 na alishika
nafasi ya kwanza katika riadha.
Mnamo mwaka 1999 alikuwamo katika orodha ya Wanariadha
bora wa karne ya 20 akishika nafasi ya sita.
Alizaliwa Septemba 12, 1913, alikuwa mtoto wa mwisho
kati ya kumi waliozaliwa kwa baba mkulima Henry Cleveland Owens na mama Mary
Emma Fitzgerald huko Oakville, Alabama. Akiwa na umri wa miaka tisa, familia
yake ilihamia Cleveland, Ohio kwa ajili ya kutafuta fursa nzuri zaidi ya kazi.
Kipindi hicho Wamarekani weusi akali ya milioni 1.5
waliokuwa wakiishi Kusini walihamia maeno ya mijini na upande wa kaskazini kwa
ajili ya shughuli za viwandani. Inaelezwa aliitwa Jesse baada ya mwalimu wake
kumuuliza jina lake ambapo aliangalia katika daftari lake la kumbukumbu na
kutamka J.C kifupisho cha James Cleveland.
Lakini mwalimu wake alifikiri kuwa James ametamka
Jesse kutokana na lafudhi ya Kusini hivyo tangu wakati huo akaanza kuitwa Jesse
badala ya James.
Enzi za uhai wake aliwahi kusema, “Niliiachia miguu
yangu muda mchache katika ardhi iwezekanavyo. From the air, fast down, and from
the ground, fast up.”
0 Comments:
Post a Comment