Machi 23, 1998 Makundi mawili ya mashabiki wa soka wa nchini Uholanzi yalipambana na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
Kundi la mashabiki wa Feyenoord lilipambana vikali na kundi la mashabiki wa Ajax Amsterdam. Feyenoord ipo jijini Rotterdam umbali wa kilometa 78.8 kusini mwa jiji la Amsterdam kiasi cha mwendo wa dakika 62 kwa gari.
Miamba hiyo ya soka imekuwa hasimu hadi kutengeneza mechi ya watani wa jadi ya De Klassikier. Katika vurugu hizo zilisababisha mtu aliyefahamika kwa Carlo Picornie kupoteza maisha. Siku hiyo hakuna aliyecheza mchezo wowote lakini tambo za hapa na pale ndizo zilizochochea mapamabno hayo.
Ilikuwa hivi mashabiki hao walikutana katika uwanja mdogo huko Beverwijk uliopo umbali wa kilometa 12 kutoka Amsterdam. Mashabiki hao walipambana kwa dakika tano lakini kutokana na kurushiwa na vitu mbalimbali kijana mmoja ambaye alikuwa shabiki wa Amsterdam alijeruhiwa na baadaye kupoteza maisha.
Taarifa za baadaye zilieleza kuwa marehemu alikuwa anafahamika kwa jina la Picornie aliyekuwa na umri wa miaka 35. Ilielezwa kuwa Picornie alikuwa baba wa watoto wawili na meneja wa hotel na kwamba aliwahi kuwa kiongozi kundi la mashabiki wa Ajax kwa miaka mingi.
Kitendo hicho kiliwakumbusha wengi nchini humo kama vurugu za mashabiki wa timu hizo mbili miaka ya 1960. Hata hivyo serikali ya nchi hizyo ilifuatilia na kuwakamata waliohusika katika vurugu hizo huku ikishindwa kuwatambua moja kwa moaja na kifo cha Picornie.
0 Comments:
Post a Comment